MBUNGE wa Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu,akiulizwa swali katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametaka kujua mpango wa serikali wa kuwapunguzia mzigo wa tozo wachimbaji wadogo wa Jimbo la Singida Mashariki ili wapate tija katika uchimbaji wao.
Mtaturu amesema hay oleo Februari 14,2025,Bungeni wakati akiuliza swali katika kipindi cha maswali na majibu.
“Mwaka 2019 vikundi vya Jimboni kwangu vilipewa leseni ambavyo ni Mang’onyi Mining,Dhahabu ni mali pamoja na Baraka Group,lakini walipewa Deposit ilikuwa mbali sana kwa hiyo wakawa hawana uwezo kwa sababu mtaji wao ni mdogo,je mko tayari kwenda kuongea na wachimbaji hao na kuwashauri jinsi ya kuweza kupata leseni nyingine waweze kupata tija,”?.
La pili,“Kuna tozo ambayo wanatozwa kama mrabaha wa wachimabji wadogo pale tu wanapokuwa wanatoa madini yao pale kwenye eneo la mgodi,wanatozwa hiyo tozo na baadae wakienda sokoni wanatozwa tena kodi ya serikali hiyo ni kama vile Double Taxation,nini mpango wa serikali wak uwapunguzia mzigo wachimbaji hawa ili wapate tija katika uchimbaji wao,?amehoji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Madini Steven Kiruswa amempongeza Mbunge Mtaturu kwa namna anavyowapambania wachimbaji wadogo.
“Mheshimiwa Mtaturu ni Mpambanaji makini katika kuwatetea wachimbaji wadogo wa Jimboni kwake na Singida kwa ujumla,amekuwa pia ni balozi mzuri katika kusaidia kutatua migogoro ya wachimbaji wadogo katika eneo lake,”amesema.
Amesema wachimbaji wadogo hao wanahitaji eneo mbadala japo kuwa ni wajibu wao kutafuta maeneo ya karibu ila wizara itakuwa tayari kuwapatia leseni kama zipo wazi.
“Nipo tayari kushirikiana nae pamoja na afisa madini mkazi wa Mkoa wa Singida kuangalia kama kuna maeneo mbadala wanayoweza kupewa wachimbaji hao wadogo wa madini,”.amesema.
Kuhusu mrabaha wanaochajiwa mara mbili amesema wachimbaji wa maduara kwenye madini ya dhahabu wanachimba kwa kushirikiana nay ale mawe yanapotolewa nje ya ardhi wanagawana na wanaweza kuwa watu 20 au 30.
Amesema wanapogawana wanatawanyika kila mtu anapeleka mahali pa kuchakatia na wanapoteza kumbukumbu inakuwa ngumu kuwafuatilia walipe mrabaha.
“Kwa hiyo inabidi yale mawe ambayo ndio yanagawanywa yaakisiwe mrabaha ambao unalingana na makisio ya yale mawe kwa kilo sio kwa thamani yake halisi,wanapochakata kwenda sokoni wanapeleka dhahabu safi iliyosafisha na ile dhahabu iliyosafishwa inakuwa imeongezeka thamani na hapo ndipo wizara inapocharge tena mrabaha sahihi kwa ile ambayo imesafisha yale madini,”amesema.
Amesema ili kuepukana na changamoto hiyo wameenda na utaratibu ambao unaendelea kutengenezwa wa kutengeneza maeneo ya kuchakata pamoja karibu na maeneo ya machimbo ili lile zao la mwisho ambalo ni dhahabu yenyewe liweze kuchajiwa mrabaha mmoja tuu na waondokane na kero hiyo.