Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano wa Kumi na Nane wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Utakaoanza siku ya Jumatano 12/02/2025 ambapo Jumla ya Miswada Miwili ya Sheria inatarajiwa kusomwa kwa mara ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Na Sabiha Khamis -Maelezo
Mkutano wa 18 wa Baraza la 10 la Wawakilishi unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano Febuari 12, mwaka huu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Katibu wa Baraza hilo, Raya Issa Mselem katika ukumbi wa Mikutano Baraza hilo Chukwani Wilaya ya Magharib B Unguja amesema mkutano huo utahusisha na kuendesha shughuli mbalimbali za Baraza ikiwemo maswali na majibu.
Amesema jumla ya maswali 190 yameratibiwa na Afisi ya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya Mkutano huo ambapo maswali hayo yatajibiwa na Serikali.
Ameeleza kuwa pia mkutano huo utajadili miswada miwili ya sheria iliyowasilisha na kusomwa kwa mara ya kwanza mwezi Disemba mwaka jana na kujadiliwa kwa mara ya pili.
Ameitaja miswada yenyewe ni mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya ununuzi na uuondoaji wa mali za umma Nam. 11 ya mwaka 2016 na kutunga Sheria mpya ya ununuzi wa umma na kuweka masharti bora ya usimamizi na udhibiti wa umma.
Aidha mswada mwengine ni mswada wa Sheria wa kufuta Sheria za Baraza la udhibiti wa mfumo wa utoaji leseni za biashara Nam. 13 ya mwaka 2013 na kutunga Sheria ya udhibitia na usimamizi wa utoaji leseni za biashara Zanzibar.
Aidha Katibu huyo amefahamisha katika mkutano kutakuwa na uwasilishaji wa ripoti za kamati za kudumu za Baraza la Wawakilishi kwa mwaka 2024 – 2025 pamoja na taarifa ya Serikali juu ya mwelekeo wa mpango wa taifa 2025 – 2026.
Mkutano huo wiki mbili ambao unatrajiwa kumalizika siku ya Ijuma Februari 28, mwaka huu.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano wa Kumi na Nane wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Utakaoanza siku ya Jumatano 12/02/2025 ambapo Jumla ya Miswada Miwili ya Sheria inatarajiwa kusomwa kwa mara ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Afisa wa Habari wa Habari Maelezo Sabiha Khamis Mgeni akifuatilia Mkutano wa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano wa Kumi na Nane wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Utakaoanza siku ya Jumatano 12/02/2025 ambapo Jumla ya Miswada Miwili ya Sheria inatarajiwa kusomwa kwa mara ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano wa Kumi na Nane wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Utakaoanza siku ya Jumatano 12/02/2025 ambapo Jumla ya Miswada Miwili ya Sheria inatarajiwa kusomwa kwa mara ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.