MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Victor Swella,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 29,2025 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha Oktoba- Disemba 2024.
Na Alex Sonna,Dodoma
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imekamata mbolea ya ruzuku ambayo ilikuwa inauzwa kinyume na utaratibu kwa wakulima kwa bei ya juu.
Hayo ameelezwa Leo Jumatano 29,2025 Jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,Bw.Victor Swella wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha Oktoba- Disemba 2024 kwa Waandishi wa Habari.
Bw.Swella,amesema Mbolea hiyo ilikuwa inauzwa Shilingi 150,000 badala ya bei elekezi ya Shilingi 75,000.
“Katika tukio hili tulifanikiwa kumkamata mfanyabiashara mmoja na kumfungulia kesi namba 32320/2024 katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma….
“Mshtakiwa alishtakiwa kwa kuuza mbolea bila kuwa na kibali na alikiri kosa hilo na Mahakama ilimtia hatiani na kumuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya Shilingi milioni 2.
Swella amesema mshtakiwa alilipa faini ya Sh milioni 2 na kuachiwa huru.