Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro amesema kuwa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia unalenga katika kutoa elimu ya Msaada wa Kisheria ili kuwawezesha Wananchi kutatua changamoto zao.
Waziri Ndumbaro amesema hayo Leo tarehe 24 Januari, 2025 katika viwanja vya Mwanga Centre Mkoani Kigoma wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Mkoani Kigoma, Wa
na amesema kuwa Kampeni hiyo inalenga kulinda na kuimarisha misingi ya Kisheria katika utatuzi wa changamoto na migogoro ya Wananchi.
Waziri Ndumbaro ametoa rai kwa Wananchi kuitumia fursa hiyo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma kwa muda wa siku tisa ili kutatua changamoto hizo ambapo amewaagiza Wasaidizi wa Msaada wa Kisheria kuwasaidia Wananchi ili kupata Suluhu katika changamoto za Kisheria zinazowakabili.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Rashid Chuachua amesema Kampeni hiyo itaongeza ufanisi na utekelezaji wa majukumu ya Kisheria ambapo amesema itasaidia katika kuleta
suluhisho na kuwa chachu ya maendeleo.
Nao baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma , Abdullah Mfaume na Leonia Chubwa wamesema ujio wa Kampeni hii ni msaada mkubwa kwako kwani walikuwa wakikosa Haki zao kwa kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya maswala ya Kisheria.
Kampeni Hii Itatekelezwa Katika Halmashauri zote nane za Mkoa Wa Kigoma ikijumuisha Kata 80 Na Vijiji Na Mitaa 240 Kwa Kipindi Cha Siku 9 Kuanzia Januari 25 Hadi Februari 02 , 2025.
Kigoma umekuwa Mkoa wa 12 ambapo kwa siku ya leo tarehe 24 Januari, 2025 Kampeni hiyo imezinduliwa katika Mikoa ya Katavi, Mtwara na Tabora, tarehe 26 Kampeni hiyo itazinduliwa katika Mkoa wa Geita na tarehe 29 Mkoani Kilimanjaro.