Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Ruth Zaipuna, Mazungumzo yaliyofanyika mkoani Dodoma.
Mazungumzo hayo yamelenga kuangazia mafanikio ya Benki ya NMB yaliyopatikana mwaka 2024 pamoja na mikakati iliyopo kwa mwaka 2025 katika kuwafikishia Watanzania wengi zaidi huduma za kibenki na kuendeleza ubunifu katika huduma hizo.