MUONEKANO wa Jengo la Wakala wa Vipimo (WMA) Makao Makuu jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,ameridhishwa na ujenzi wa Jengo la Wakala wa Vipimo (WMA) Makao Mkuu Dodoma huku akimpongeza Mkandarasi kwa kujenga katika kiwango chenye ubora mkubwa.
Dkt.Abdallah ametoa pongezi hizo leo Januari 20,2025 jijini Dodoma mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Amesema matarajio yao ni kuona mradi huo unakamilika kwa wakati huku akiridhishwa na ubora wa jengo hilo.
“Nimeridhishwa na utendaji kazi wa WMA kwa kazi yenu nzuri ya kumsimamia Mkandarasi kwa kujenga katika kiwango bora pia nimpongeze Mknadarasi kwa kasi anayoendelea nayo katika kujenga hili jengo ambalo litasaidia kuboresha ufanisi wa kazi litakapokamilika”amesema Dkt.Abdallah
Hata hivyo Dkt.Abdallah,amesema maboresho ya kutoa huduma bora ni pamoja na kuwa na mazingira mazuri kama ujenzi wa majengo ya kisasa.
“Tumeona mambo ya msingi yamekamilika na mwezi wa pili jengo atakabidhi kwa WMA ,nimejionea kila sehemu ambazo ni muhimu kuwa jengo limejengwa katika ubora wenye viwango,”amesema
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo Bw. Alban Kihulla,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa jengo la kisasa ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 95.2 uweze kukamilika.
Bw.Kihulla amesema dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona wanafanya kazi katika mazingira mazuri na yenye ubora ndio maana akatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la Wakala huo Jijini hapa.
Amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza Julai 2,2022 ambapo matarajio ni kukamilika mwaka 2024 hata hivyo wameongeza muda kutokana na mkandarasi kupata changamoto mbalimbali.
Amesema matarajio ujenzi huo ukamilike February 10 mwaka huu na umefikia asilimia 95.2 ambapo gharama za ujenzi ni Sh bilioni 6.2 na mpaka sasa wamelipa Shilingi bilioni 5.8.
“Ni matarajio yetu nae mkandarasi atakamilisha kwa wakati ili tuanze sasa kulitumia jengo hili.Kupitia jengo hili naaamini tutazidi kuboresha huduma zetu na zitazidi kuwa na ubora,”amesema Bw.Kihulla
Naye Mkandarasi wa Kampuni ya Mohamed Builders Bw.Burhan Hamza,ameipongeza WMA kwa kumpa kazi hiyo huku akiahidi kuwa mradi huo watakabidhi Februari 10 mwaka huu.
Amesema ujenzi ulitakiwa kuisha Desemba 30 mwaka jana ila waliomba siku 40 kutokana na kutokea kwa changamoto mbalimbali.
“Changamoto tuliyokutana nayo ni kuagiza vifaa kutoka nje ya Tanzania hivyo kushindwa kuvipata kwa wakati ndiyo maana wameomba siku 40 na wiki hii vifaa vyote vitakuwa vimeingia nchini na kazi itaendelea kama kawaida”amesisitiza
Awali Mwakilishi wa Msimamizi wa Mradi Bi.Rachel Lister ,amesema wanaendelea kusimamia ujenzi huo na wapo katika hatua za mwisho na imani yao ni kukamilisha kwa wakati.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bw.Alban Kihulla,wakati wa ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma leo Januari 20,2025 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya Mohamed Builders Bw.Burhan Hamza,mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma leo Januari 20,2025 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah,akiendelea kukagua ujenzi wa Jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma leo Januari 20,2025 jijini Dodoma.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la WMA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma leo Januari 20,2025 jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bw.Alban Kihulla,akielezea ujenzi wa jengo hilo ulipofikia mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,kufanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Jengo la WMA Makao Mkuu Dodoma leo Januari 20,2025 jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Jengo la Wakala wa Vipimo (WMA) Makao Makuu jijini Dodoma.