RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), utakaofanyika mwezi Februari mwaka huu Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa ALAT,Taifa Murshid Ngeze, alibainisha hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Kamati tendaji kwa ajili ya kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo mkutano mkuu wa mwaka wa Jumuiya hiyo.
Ngeze, alisema mkutano huo ambao ni wa mwisho kwenye uongozi wao umepangwa kufanyika jijini Mwanza mwezi ujao ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
“Nigusie kuhusu mkutano wetu wa mwisho katika uongozi wetu ambao tulimwalika mweshimiwa Rais kuwa mgeni rasmi hapa nimwagize katibu kuhakikisha kuwa mambo yote yanayohusu mkutano huu yanakuwa sawa ili tumwandikie barua ya kumkumbusha Rais kwa ajili ya kuwa mgeni rasmi”alisema
Aidha, alisema ili kufanyikisha mkutano huo mshikamano ndani ya Jumuiya hiyo ni muhimu kwakuwa hakuna taasisi ambayo inaweza kuendelea bila kuwa na umoja.
“Nipongeze kwa mshikamo uliopo baini yetu naomba uendelee taasisi yoyote ili iendele lazima muwe na mshikamo bila mshikamno hatuwezi kwenda mbele nawashukuru sana kwa namna ilivyo sasa,”alisema
Vile vile, alisema ili kuimarisha mahusiano ya nadi na je ya Jumuiya hiyo Katibu anapaswa kuanadika baruka katika nchi mbili ambazo Kamati tendaji ianweza kujigawa kwa ajili ya kufanya ziara ya kwenda kuimarisha mahusiano.
“Katibu andika nchi mbili ambazo Kamati inaweza kujigawa ikaenda kutembelea na kumarisha mahusiano hata kama haitafanyika hivi sasa wakati wa uongozi wetu lakini mapendekezo yawepo kwa ajili ya kwenda kuimarisha mahusiano”alisema
Naye Katibu Mkuu wa ALAT, Mohammed Maje, alisema katika kupanua wigo wa mahusiano wanatarajia kukutanao na Balozi mbalimbali nchini ikiwemo wa Denmark, Sweden na Marekani.
Kadhalika, alisema tayari wamepeleka taarifa za kueleza kuwa Jumiya ya ALAT ni nini, lakini pia kuwaeleza mahusiano na Mamlaka za serikali za Mitaa.
Hata hivyo, alisema ajenda za kiako hicho ni pamoja na kufungua kikao,kuthibitisha ajenda,kusoma na kuthibitisha mukhutasari wa kikao kilichopita, kusoma mapato na matumizi, taarifa ya utekelezaji wa shughuli za ALAT pamoja na mengineyo.