TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
(i) Mhandisi Ramadhani Masoud Lwamo ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Lwamo alikuwa akikaimu nafasi hiyo;
(ii) Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) kwa kipindi cha pili;
(iii) Prof. Othman Chande Othman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili;
(iv) Dkt. Florens Martin Turuka ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa kipindi cha pili; na
(v) Prof. Valerian Cosmas Silayo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kwa kipindi cha pili.