RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kizimbani hadi Kiboje na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohammed (kushoto) ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo 2-1-2025, katika eneo la Kizimbani.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akikagua ujenzi wa Barabara ya Kizimbani hadi Kiboje, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo leo 2-1-2025, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MUONEKANO wa Barabara ya Kizimbani hadi Kiboje inayojengwa kwa kiwango cha lami iliyoweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo leo 2-1-2025 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
VIJANA wa Kikundi cha uhamasishaji wakishangilia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Barabara ya Kizimkazi hadi Kiboje, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichan) akizungumza na Wananchi katika kiwanja cha mpira Kiboje leo 2-1-2025, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)