Vijana wanaotumia muda mwingi vijiweni wakipiga soga na kucheza michezo ya bao wametakiwa kutumia muda mwingi kufanya kazi zitakazo waingizia kipato na sio kutumia muda mwingi vijiweni kuanzia asubuhi hadi jioni kwani kitendo hicho kitawapelekea kufanya uhalifu kutokana na kukosa kipato halali.
Hayo yalisemwa Januari 02, 2025 na Polisi kata ya Mahenje Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Nelson Mwinuka alipotembelea maeneo mbalimbali ya vijiwe vya michezo ya Bao na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kutumia muda wao kwenye kazi za maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.
Sambamba na hilo, Mkaguzi Mwinuka aliwataka wananchi hao kujiepusha na vitendo vya ukatili ikiwemo na kuwapatia haki ya elimu watoto wao ikiwa ni sambamba na kutenga muda mchache wa kujiburudisha katika michezo mbalimbali na kuwa na tabia ya kufichua wahalifu pamoja na kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.
ReplyReply to allForward |