Mhandisi James Jumbe (katikati) akizungumza wakati akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Katika kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025, Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe, ameongeza furaha kwa makundi maalum katika Manispaa ya Shinyanga kwa kuwapatia zawadi za vyakula.
Zawadi hizo zimetolewa kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre, Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, pamoja na mabinti waliopitia changamoto za ukatili wa kijinsia wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Vyakula vilivyotolewa ni pamoja na mbuzi wawili kwa kila kituo, mchele, unga wa ngano, mafuta ya kula, maharage,sukari, sabuni za kufulia, na vinywaji, ikiwa ni pamoja na maji na juisi kama sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025.
Mhandisi Jumbe amekabidhi zawadi hizo leo, Desemba 31, 2024 kwa furaha na kusema kwamba ni muhimu kuyakumbuka makundi haya maalum muda wote lakini hasa wakati wa sherehe kama za Sikukuu ya Mwaka Mpya.
“Katika kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya, nimeona nisiyaache nyuma makundi maalum. Nimekuja na zawadi mbalimbali ikiwemo mbuzi, mchele, sukari, mafuta ya kula, maharage, sabuni na vinywaji.
Nimefika katika vituo hivi ili kusherehekea na makundi haya maalum, kwani ni muhimu kuwafariji na kuwapatia mahitaji yanayotakiwa. Hii siyo mara ya kwanza, mwaka uliopita nilileta mahitaji kupitia wawakilishi wangu. Na safari hii siyo ya mwisho, nitaendelea kutoa misaada na kuwatia moyo. Naomba wadau wengine wajitokeze kusaidiana na Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa bega kwa bega na makundi haya,” amesema Mhandisi Jumbe.
“Lazima tuwatunze wazee wetu na pia tusikie kilio cha watoto ambao wamepitia changamoto mbalimbali katika maisha. Ni muhimu kuwapa furaha na kuhakikisha wanapata mahitaji yao muhimu, ili tuwe na taifa lenye upendo, umoja, na mshikamano”,ameongeza Mhandisi Jumbe.
Mhandisi Jumbe amewahimiza wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kujitolea kusaidia makundi haya maalum, akisema kwamba kila mmoja anawajibika katika kusaidia jamii hasa wale wanaokumbwa na changamoto kubwa katika maisha.
Sehemu ya mbuzi waliotolewa na Mhandisi James Jumbe.
Wakizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, watoto na wazee akiwemo Ansita Francis, Catarina Maige na Kija Nipuge wametoa shukrani zao kwa Mhandisi Jumbe kwa msaada huo mkubwa, ambao unawapa furaha ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya.
“Asante baba Jumbe kwa zawadi hizi. Mungu akubariki kijana wetu. Hatukutegemea kama tutapata chakula cha Sikukuu, lakini leo tumeweza kusherehekea kwa furaha, tumepata mchuzi na nyama, na tunashukuru sana”, amesema Mzee Kija Nipuge, ambaye ni mzee wa Makazi ya Wazee ya Kolandoto.
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe (kulia) akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP), linalosimamia Kituo cha kulelea mabinti waliopitia ukatili wa kijinsia katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School, Yohana Hezron, pamoja na Mkurugenzi wa Shinyanga Society Orphanage Centre, Bi. Ayam Ally Said, wamemshukuru Mhandisi Jumbe kwa msaada wake endelevu kwa makundi maalum.
“Tunashukuru sana kwa msaada huu. Zawadi hizi zitasaidia sana makazi yetu. Tunaomba wadau wengine waendelee kutembelea vituo vyetu na kutoa msaada ambao utatatua changamoto zinazowakabili watu hawa”,amesema Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Sophia Kang’ombe.
Vilevile, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe, amesema kwamba Mhandisi Jumbe ni mfano bora wa kusaidia makundi maalum na ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia, mfano kwa Kituo cha Agape, ambacho kinahitaji nishati mbadala ili kuondokana na matumizi ya kuni wakati wa kupikia.
Amesema kuwa, msaada wa nishati mbadala utasaidia kupunguza muda wanaopoteza kutafuta kuni na kuwawezesha mabinti hao kupata muda zaidi wa masomo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Sehemu ya mbuzi waliotolewa na Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre, Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, pamoja na mabinti waliopitia changamoto za ukatili wa kijinsia wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School ili kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akisamiliana na Mkurugenzi wa Shinyanga Society Orphanage Centre, Bi. Ayam Ally Said alipotembelea kituo hicho cha kulelea watoto yatima kwa ajili ya kutoa zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025.
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre kilichopo Bushushu kata Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe (katikati) akizungumza wakati akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre kilichopo Bushushu kata Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre kilichopo Bushushu kata Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre kilichopo Bushushu kata Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Sehemu ya zawadi zilizotolewa kwa Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre
Mmoja wa watoto akitoa neno la shukrani kwa Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe.
Mkurugenzi wa Shinyanga Society Orphanage Centre, Bi. Ayam Ally Said akizungumza wakati Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe (katikati) alipotembelea kituo hicho cha kulelea watoto yatima kwa ajili ya kutoa zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025. Mkurugenzi wa Shinyanga Society Orphanage Centre, Bi. Ayam Ally Said (wa pili kulia) akizungumza wakati Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe alipotembelea kituo hicho cha kulelea watoto yatima kwa ajili ya kutoa zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025.
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Sophia Kang’ombe akitoa neno la shukrani baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Sophia Kang’ombe akitoa neno la shukrani baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe, akizungumza baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Catarina Maige akitoa neno la shukrani baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Kija Nipuge akitoa neno la shukrani baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Kija Nipuge akitoa neno la shukrani baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa mabinti wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe (aliyevaa kanzu) akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa mabinti wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe (aliyevaa kanzu) akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa mabinti wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe (aliyevaa kanzu) akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa mabinti wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Sehemu ya zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa mabinti wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.Sehemu ya zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025 kwa mabinti wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School. Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe akisaini kitabu cha wageni katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akitoa neno la shukrani baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP), linalosimamia Kituo cha kulelea mabinti waliopitia ukatili wa kijinsia katika Shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School, Yohana Hezron akitoa neno la shukrani baada ya Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2025