Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Dk, Mwalim Haroun Ali Suleiman kulia akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara za Muungano,Jango’mbe,Miembeni ,Kidongochekundu,Mental Hospitali na za karibu yake Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi Amani Umoja na Msikamano kwa Maendeleo yetu.
Baadhi ya wageni waalikwa na Wafanyakazi waliohudhuria katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara za Muungano,Jango’mbe,Miembeni ,Kidongochekundu,Mental Hospitali na za karibu yake Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi Amani Umoja na Msikamano kwa Maendeleo yetu.
Baadhi ya Vijana wahamasa wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara za Muungano,Jango’mbe,Miembeni ,Kidongochekundu,Mental Hospitali na za karibu yake Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi Amani Umoja na Msikamano kwa Maendeleo yetu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Habiba Hassan Omar akitoa hotuba ya Kitaalamu katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara za Muungano,Jango’mbe,Miembeni ,Kidongochekundu,Mental Hospitali na za karibu yake Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi Amani Umoja na Msikamano kwa Maendeleo yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Dk, Mwalim Haroun Ali Suleiman akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara za Muungano,Jango’mbe,Miembeni ,Kidongochekundu,Mental Hospitali na za karibu yake Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi Amani Umoja na Msikamano kwa Maendeleo yetu.
Na Rahma Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Dk Haruon Ali Suleiman wananchi wa Jimbo la Jang’ombe kuitunza miundombinu ya barabara inayojengwa ili idumu kwa muda mrefu.
“Miundombinu yetu hii tuitunze kwa maslahi ya Nchi yetu na vizazi vyetu vijavyo” alisema Dkt Haroun.
Aidha amewataka Wakala wa barabara kuendelea kuziboresha barabara zinazojengwa na endapo itatokea uharibifu katika miundombinu hiyo wasisubiri na badala wake kurekebisha hitilafu zilizopo ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.
Wito huo ameutoa Jang’ombe Matarumbeta alipokua akiweka Jiwe la Msingi katika barabara ya Jang’ombe, Miembeni, Muungano Kidongo chekundu ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za kutimiza miaka 61 ya Mapinduzi a Zanzibar.
Amesema Mapinduzi yamekuja kuibadilisha Zanzibar kimaendeleo pamoja na kulinda Amani na utulivu uliopo nchini.
Akitoa taarifa ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa barabara hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt Habiba Hassan Omar amesema kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi na ni dira ya mpango wa maendeleo pamoja na usafiri.
Mei 2022 na zinatarajiwa kukamilika Mei 20225 ambapo umezingatia kuweka mitaro ya kupitisha Maji pamoja miundombinu yote ya barabara ikiwemo watu wenye mahitaji maalum
Ameongeza kuwa ujenzi wa barabara hizo umegharimu Dola za kimarekani Milioni 3.64 ikiwa ni gharama za ujenzi huo zinajumuisha barabara kuu ambazo zina upana wa kilomita 8 na barabara za ndani zenye wastani wa mita 4
Akitoa salamu za Mkoa wa Mjini Magharib Mkuu wa Wilaya ya Mjini Hamid Seif Said amesema kuwa Mkoa uko salama kwani wananchi wake wanaendelea na shughuli zao za kimaendeleo bila ya wasiwasi.
Aidha amesema kuwa kuweka Jiwe la msingi katika barabara hizo ni zenye urefu wa kilomita 4.9 ni kuadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi.
Ujenzi wa barabara hizo zilianza rasmi arehe 1 Disemba 2022 baada ya malipo ya awali kwa muda wa utekelezaji wa miezi 36 chini ya Mshauri Elekezi Dalhandaz kutona Lebanon.