Katika kuadhimisha sikukuu za mwisho wa mwaka zinazoendelea, Mgodi wa Barrick North Mara, umetoa zawadi kwa makundi mbalimbali yenye mahitaji kwenye jamii katika wilaya za Tarime na Serengeti ikiwemo vituo vya kulea watoto yatima, na wazee wa kimila ili kuwezesha makundi hayo kusherekea kwa furaha sambamba na kudumisha uhusiano mwema.
Wazee wa kimila kutoka koo 12 wamekabidhiwa zawadi mbalimbali za sukari, mchele,mafuta ya kupikia na Ng’ombe wa kitoweo ili washerehekee sikukuu na wanaukoo wenzao katika vijiji wanavyotoka.
Mgodi wa North Mara kila mwaka umekuwa na utamaduni wa kukumbuka makundi mbalimbali kwenye jamii na kuyapatia zawadi mbalimbali wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya hususani vituo vya kulea watoto yatima na wenye changamoto za kijamii,wagonjwa na wazee wa mila kutoka vijiji mbalimbali vinavyozunguka mgodi huo.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha ATFGM Masanga wilayani katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Barrick North Mara baada ya mgodi huo kukabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu kwenye kituo hicho.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Masanga wakifurahia zawadi wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi za Sikukuu.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Wazee wa kimila wakifurahia zawadi mbalimbali baada ya kukabidhiwa walipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa mgodi huo
Wazee wa kimila wakifurahia zawadi mbalimbali baada ya kukabidhiwa walipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa mgodi huo