Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thatib Kombo amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Sweeden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam Desemba 23, 2024.
Akipokea nakala hizo Waziri Kombo amempongeza Mhe. Macias kwa uteuzi aliuopata na amemuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi atakachokuwa nchini kuiwakilisha nchi yake.
Aidha, Mhe. Kombo ameishukuru Serikali ya Sweeden kwa mchango wake katika uboreshaji wa Mahakama nchini, mifumo ya utoaji huduma za afya nchini na kuimarisha utawala bora; hatua ambayo imekuza uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Balozi Macias amesema Sweeden itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika maeneo mbalimbali yakiwemo biashara na uwekezaiji, nishati, usafiri, afya na mabadiliko ya kijani.