Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewasili jijini Oslo, Norway kwa ziara yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Norway pamoja na nchi za Nordic.
Mara baada ya kuwasili, Mhe. Kombo amekutana na ujumbe wa Tanzania kwa maandalizi ya Awamu ya Nne ya Mashauriano ya Kisiasa Baina ya Tanzania na Norway (The 4th Tanzania – Norway Political Consultation).
Aidha, Mhe. Waziri Kombo atashiriki katika Mkutano wa 23 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Nordic na Afrika (Nordic-Africa Foreign Ministers’ Meeting) utakaofanyika Novemba 19 na 20, 2026.
Kaulimbiu ya Mkutano huo ni ‘Dialogue in an Era of Uncertainty. United for a Prosperous Future’ (Mjadiliano katika Zama za Kutokuwa na Hakika. Muungano kwa kesho yenye Ustawi).
Jumla ya nchi 30 za Afrika zinatarajiwa kuwa na uwakilishi katika mkutano huo.

