Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 05.12.2024 imetoa elimu kwa Umoja wa Wajane Arusha juu ya mbinu za kuwaepusha watoto wao na tatizo la dawa za kulevya katika Uwanja wa Shk. Amri Abeid Karume jijini Arusha.
Wajane hao zaidi ya 250 walifundishwa dalili za kutambua kama watoto wao wameshaanza kujihusisha na dawa za kulevya. Pia, walielekezwa uhusiano uliopo kati ya dawa za kulevya na afya ya akili.
Umoja huo ulihamasishwa kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya katika maeneo yao kwa kupiga namba ya simu ya bure 119.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241209-WA0109-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241209-WA0111-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241209-WA0112-1024x682.jpg)