Naibu waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia, na makundi maalumu Mwanaidi Ali Hamisi akizungumza katika.mahafali.hayo chuoni hapo .
Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Bakari George akizungumza katika.mahafali hayo mkoani Arusha .
Happy Lazaro,Arusha .
Naibu waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia, na makundi maalumu Mwanaidi Ali Hamisi amesema kuwa wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa Chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru katika kuboresha miundombinu ili kiendelee kutoa huduma bora kwa jamii.
Ameyasema hayo mkoani Arusha kwa niaba ya Waziri Dorothy Gwajima wakati akizungumza kwenye mahafali ya 18 chuoni hapo ambapo jumla ya wanafunzi 1,652 wamehitimu shahada za Uzamili,shahada za kwanza,Stashahada,na Astashahada.
Mwanaidi Ali amesema kuwa ,wizara itaendelea kutoa ushirikiano ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili chuo kwa sasa .
“Nimefurahishwa pia na mipango mbalimbali ambayo mmejiwekea,ni wazi kuwa kutekelezwa kwa mipango hiyo kutaleta mabadiliko makubwa ,hivyo naomba chuo kiandae mpango kazi na kuwasilisha wizarani ili na sisi tuweze kufuatilia na kushirikiana nani katika utekelezaji. “amesema .
Amefafanua kuwa, serikali.ya awalu.ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo mkubwa sana katika uendelezaji na uimarishaji wa sekta ya maendeleo ya jamii,kama mnavyojionea jitihada kubwa zimefanyika na kinaendelea kufanyika katika uimarishaji wa huduma za jamii kama vile elimu,afya,maji,na barabara.
“Mhe Rais amekuwa kinara wa kusisitiza na kutekeleza kwa vitendo falfasa ya maendeleo ya jamii kwa kuhimiza ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli na miradi ya maendeleo “
“Jamii zetu bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukatili wa kijinsia,ukatili dhidi ya watoto,mabadiliko ya tabia nchi na mmomomyoka wa maadili,hivyo ninyi mnazo nyenzo za kugeuza changamoto hizi kuwa fursa kwa afua mbalimbali za utatuzi kwani kwa kufanya hivyo sio tu mtaweza kujiajiri bali mtakuwa mmetoa mchango wenu wa moja kwa moja kwa Taifa letu.”amesema
Naye Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Bakari George amesema kuwa,sherehe za mahafali hutanguliwa na maadhimisho ya wkiki ya maendeleo ya jKatika kipindi cha mwaka 2024/ 25 Taasisi kimeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kujibu wa mpango mkakati wa Taasisi wa miaka mitano 2023/24-2027/2028 ambapo mambo mbalimbali.yamefanyika kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 ikiwemo ukuaji wa bajeti katika.kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2021/2022 hadi 2023/2024 .
Amesema kuwa ,sherehe za mahafali hutanguliwa na maadhimisho ya wiki ya maendeleo ya jamii na ubunifu ambapo kwa mwaka huu chuo kimeadhimisha wiki hii kuanzia desemba 2 hadi kilele chake ambapo ndio sherehe za mahafali yao ambapo kauli mbiu ilikuwa “Maendeleo ya jamii na ubunifu 2024.
Amesema kuwa, chuo kinatambua umuhimu wa ubunifu , ujasiriamali, michezo,na burudani katika kupunguza utegemezi wa wahitimu wa vyuo vikuu kwenye ajira rasmi.
“Katika kipindi cha mitatu kuanzia mwaka 2021/2022 hadi 2023/2024 Taasisi imeshuhudia ukuaji wa bajeti mwaka hadi mwaka amapo wakati mwaka wa fedha 2021/2022 bajeti ilikuwa shilingi 6,082,801,175.00 kwa mwaka 2023/2024 iliongezeka na kumefikia kiasi cha shilingi 11,016,545,614.00 ambayo ni sawa na ongezeko la bajeti kwa asilimia 81 .”amesema .
Amefafanua kuwa, utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la ghorofa tatu ( sakafu nne ) ambalo lina jumla ya ofisi 44 , kumbi tano za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua watu 545 kwa wakati mmoja hadi kukamilika kwake ,ambapo mradi huu unaotekezwa kwa fedha za maendeleo kutoka Serikali kuu , unatarajia kutumia kiasi cha shilingi 5,664,000,000.00 . Hatua iliyofikiwa kwa mradi huo wa ujenzi ni hatua ya boma sakafu ya tatu ( ghorofa ya pili ) sawa na asilimia 45 ya ujenzi .
Kwa upande wake Mmoja wa washiriki katika mahafali hayo Esta Laizer mhitimu wa digrii ya maendeleo ya jamii amesema kwa, anashukuru chuo hicho kwa namna ambavyo kimeweza kuwaandaa wanafunzi kuweza kujiajiri ambapo watatumia elimu.waliyoipata kusaidia jamii kuibua matatizo na kuangalia njia za kutatua matatizo hayo kwa kushirikiana na serikali.