MEYA wa jiji la Arusha,Maximillian Iranghe akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha .
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .MEYA wa jiji la Arusha,Maximillian Iranghe amewataka wananchi jijini Arusha kuendelea kuwa na imani na serikali yao kwani bado inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali.ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wake.
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ,serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa vyumba vya madarasa, kujenga na kuboresha vituo vya afya.
Iranqhe amesema kuwa, baraza la madiwani lililofanyika Novemba 6 jijini hapa limeazimia manunuzi ya greda na mitambo kwa ajili ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara na mitaro inayoendelea, ambapo imetengwa kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya manunuzi ya mitambo husika .
Aidha ameongeza kuwa, baraza limeelekeza utoaji wa vibali vya ujenzi unaozingatia sheria pamoja na maendeleo ya mji, sehemu ya jiji ambayo ina mitaa kuu ya biashara na majengo makuu ya umma ikijumuishwa na viwanda, makazi, biashara, utawala na matumizi .
“Baraza la madiwani limeazimia upangaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza, uzingatie umbali na urahisi wa usafiri ili kupunguza adha kwa wanafunzi na kuboresha kiwango cha elimu na ufaulu, miradi ya ujenzi wa madarasa kukamilika kwa wakati, sambamba na ujenzi wa vivuko ili kuunganisha mitaa ya jiji na kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla” amesema Iranqhe.
Amefafanua kuwa, baraza limeelekeza uitishwe mkutano wa dharura wa baraza la madiwani kwa kuwashirikisha TARURA TANROADs na AUWSA ili kujadili kwa kina changamoto ya barabara kwenye mitaa ya jiji la Arusha na kuweza kutatuliwa kwa wakati ili.wananchi waweze kuondokana na changamoto hiyo.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na kupanda miti, kufanya usafi katika maeneo yao, wadau wa maendeleo kuendelea kufunga taa walau mbili mbele ya ofisi au makazi yao na kupamba mji kwa miti ya krismas msimu huu wa sikukuu.