Kamishna Msaidizi Idara ya Sera na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi Kanda ya Dar es Salaam Bw. William Mhoja akitoa ufafanuzi kwa Wadau wa Sekta mbalimbali (hawamo pichani) waliohudhuria kwenye Kongamano la Kodi kikanda Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli na kushoto ni Makamu wa Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo- TCCIA Bw. Boniface Ndego.
Na Eva Ngowi- WF -Dar es Salaam
Kuanzishwa kwa Kongamano la Kodi Kikanda kumeleta tija katika maboresho ya mfumo wa kodi ambapo katika maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 ushirikishwaji wa wadau uliongezeka zaidi.
Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Sera na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi Kanda ya Dar es Salaam, Bw. William Mhoja katika ufunguzi wa Kongamano la mwisho kikanda, lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Bw. Mhoja alisema malengo ya Makongamano haya ni pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji, kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali kama Utalii, Kilimo, Madini, Viwanda, Uvuvi na Ufugaji, kulinda viwanda vya ndani, kuvutia mitaji na uwekezaji nchini, kuongeza ushindani wa viwanda vya ndani, kuchochea ulipaji kodi kwa hiari na kuboresha usimamizi na ukusanyaji wa kodi, ada na tozo mbalimbali.
Kwa upande wa Mshauri wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo -TCCIA na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania- VoWET, Bi. Maida Waziri, alisema anaishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwashirikisha wadau kuweza kushiriki katika Makongamano haya ya Kodi Kikanda kwani itasaidia sana Wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kuweza kuleta mabadiliko katika Bajeti ijayo 2025/26.
“Tunaishukuru sana Serikali kupitia TCCIA kwa kufanya Kongamano hili la wazi la kujadili kuhusiana na mambo yanayohusu kodi, na Serikali tunaishukuru sana kwa kuweza kuona kuna umuhimu wa kuwashirikisha wadau ili kuleta mabadiliko ya 2025/26 katika bajeti inayokuja tunaishukuru sana, kwani; Tumeweza kutoa kero zetu na changamoto tulizokuwa nazo kama wajasiriamali na pia sisi ndio tunachangia Pato la Taifa katika nchi hii. Tumekuwa na mjadala mkubwa sana ambao umehusisha wafanyabiashara na watu kutoka Ofisi ya Hazina, TRA, na wafanyabiashara ambao tumejadili mambo mbalimbali, Alisema Bi. Waziri.
Naye Makamu wa Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo- TCCIA, Bw. Boniface Ndego alisema anaishukuru Wizara ya Fedha kwa kuwapa heshima TCCIA kudhamini Makongamano haya ambapo imefanyika mikutano nane Kikanda kwa ajili ya kuwapa fursa Wajasiriamali wadogo, Makampuni makubwa, Wafanyabiashara wa kati, Vijana,Taasisi za Elimu na Sekta nyingine kuweza kutoa maoni yao.
Makongamano haya ya Kodi kwa mwaka huu wa 2023/2024 yamefanyika katika Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Kaskazini Arusha, Kanda ya Ziwa Mwanza na Kigoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya na Iringa, Kanda ya Kusini Mtwara na kumalizika katika Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Idara ya Sera na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi Kanda ya Dar es Salaam Bw. William Mhoja akitoa ufafanuzi kwa Wadau wa Sekta mbalimbali (hawamo pichani) waliohudhuria kwenye Kongamano la Kodi kikanda Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli na kushoto ni Makamu wa Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo- TCCIA Bw. Boniface Ndego.
Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwa Wadau wa Sekta mbalimbali (hawamo pichani) waliohudhuria kwenye Kongamano la Kodi kikanda Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam, Kulia kwake ni Kamishna Msaidizi Idara ya Sera na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi Kanda ya Dar es Salaam, Bw. William Mhoja pamoja na Makamu wa Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo- TCCIA Bw. Boniface Ndego na kushoto kwake ni Mshauri wa TCCIA na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania- VoWET Bi. Maida Waziri.
Mshauri wa TCCIA na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania- VoWET Bi. Maida Waziri (aliyesimama) akitoa maoni kuhusiana na Wakandarasi wakubwa pamoja na kuwaomba TRA kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali kuhusu namna ya kutumia mifumo ya kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli na kulia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania Bw. Leodegar Tenga. Wakiwa katika Kongamano la Kikanda la Kodi, Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara kutoka Kampuni ya Bonafides Voyage Ltd. Bi. Ranjan Suchak akitoa maoni yake kuhusiana na maboresho ya kodi katika Bajeti ijayo 2025/2026 wakati wa Kongamano la Kikanda la Kodi, Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)