Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zahor Kassim Alharous akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafuta na Gesi asilia hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafuta na Gesi asilia hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zahor Kassim Alharous akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafuta na Gesi asilia hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi asilia (WUBU) Mhandisi Mwadini Juma Khatibu akitoa mada kuhusiana na hali ya utafutaji wa mafuta na Gesi asilia katika mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafuta na Gesi asilia hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR
NA MAELEZO
Serikali imedhamiria kuendeleza uwekezaji katika Sekta ya Mafuta na gesi ili Wananchi waweze kunufaika na Rasilimali zilizopo nchini.
Hayo yamezungumzwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zahor Kassim Alharous wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa habari juu ya masuala ya Mafuta na gesi asilia hafla ambayo imefanyika huko katika ukumbi wa Zura uliopo maisara Wilaya ya Mjini.
Amesema Sekta ya Mafuta na gesi asilia ni muhimu katika kuongeza ajira na kuboresha maisha hivyo Serikali inaendelea na mchakato wa utafutaji wa mafuta na gesi asilia pamoja na kutafuta wawekezaji wa kuendeleza sekta hiyo.
Amewataka Wandishi wa habari Nchini kutoa taarifa sahihi kuhusu utafutaji na uchimbaji wa mafuta ili wananchi wapate uelewa mzuri na kuondokana na wasiwasi juu ya mchakato huo.
Akitoa mada katika Mafunzo hayo Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Mhandisi, Mwadini Juma Khatib amesema Serikali imezindua Vitalu Vinane (8) vya Mafuta ambapo hatua inayofata ni kupokea maombi ya kampuni mbalimbali kuwekeza katika vitalu hivyo.
Ameongeza kuwa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta ni mchakato unaochukua muda mrefu katika utekelezaji wake hivyo amewataka Wananchi kuendelea kuwa na subira wakati wa uendelezaji wa mchakato huo.
Akifunga Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Salum Ramadhan Abdallah amewataka Maafia habari pamoja na Waandishi wa Habari Kuitumia Idara hiyo ili kuleta usimamizi mzuri wa Habari Nchini.
Aidha amewataka maafisa wa habari kuiga mfano wa wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kwa kuonesha mfano katika kuandaa mafunzo hayo kwani wao wameitumia Idara ya Habari Maelezo katika kuandaa na kuratibu mafunzo hayo.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza Wizara hiyo kwa kuwapatia mafunzo kuhusu Mafuta na Gesi asilia jambo ambalo litawarahisishia kutoa uelewa kwa Wananchi katika mambo hayo.