NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Dkt Charles Mahera akifunga mafunzo hayo mkoani Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .NAIBU Katibu Mkuu -Elimu ,wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Dkt Charles Mahera amewataka wathibiti ubora wa shule nchini kutumia maarifa,ujuzi na ubunifu waliopata katika mafunzo ya Amali ili mtaala wa elimu ya Amali sekondari ulete tija.
Dkt Mahera ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akifunga mafunzo ya wathibiti ubora wa shule nchi nzima yanayohusu tathmini ya mkondo wa Amali kwa shule za sekondari yaliyokuwa yakifanyika mkoani Arusha.
Dkt Mahera amesema kuwa,mafunzo haya yalilenga kuwawezesha kujengewa uwezo katika eneo la amali kwa lengo la kuwawezesha kufanya tathmini ya elimu.ya Amali kwa.ufanisi ili kukidhi mahitaji ya mabadiliko na mageuzi makubwa yaliyofanywa na serikali katika mtaala wa elimu ya sekondari hasa katika eneo la Amali.
Amesema kuwa,mageuzi hayo ya kielimu yanalenga kutoa elimu bora kwa kuandaa wahitimu wenye ujuzi,maarifa,stadi,ubunifu na mwelekeo chanya na wanaoweza kujiajiri au kuajiriwa ,na hivyo kukidhi mahitaji ya soko la ajira lililopo nchini kikanda na kimataifa .
“Nimetaarifiwa kuwa mliwezeshwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpangilio na maudhui ya mtaala wa Amali,fani za Amali zinazofundishwa katika shule za sekondari zenye mkondo wa Amali ,masomo yatakayofundishwa taika mkondo wa Amali,utaratibu wa kusajili shule za sekondari za Amali,mambo ya kuzingatia wakati.wa kufanya tathmini za jumla na ufuatiliaji na miaalum na muundo wa taarifa za utekelezaji wa mafunzo ya Amali.”amesema Mahera.
Aidha amewataka kutambua kuwa wao kama maafisa udhibiti ubora wa shule wana jukumu kubwa la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa katika asasi zote za elimu nchini ili kujiridhisha kama utekelezaji unafanyika kama ilivyokusudiwa na serikali na hiyo inajumuisha uzingatiaji wa sheria,kanuni,taratibu,na miongozo iliyotolewa na serikali .
Mahera amewataka kutumia maarifa,ujuzi na ubunifu wote walioupata katika mafunzo hayo kwa kutekeleza kwa vitendo katika kuwawezesha wadau wote wa elimu waliopo kwenye maeneo yanayowazunguka ili utekelezaji wa mtaala wa elimu ya Amali sekondari ulete tija kwa Taifa na kuhakikisha kwenye vyuo wanasaidia uwepo wa elimu ya Amali kwa kuwaelimisha wanajamii kufahamu umuhimu wake .
Naye Kaimu Mkurugenzi wa wathibiti ubora, Monica Mpululu amesema kuwa mafunzo hayo wataenda kuyatumia kwa ufanisi ili yalete tija kwenye mkondo wa Amali na kutoa elimu kuhusu mkondo huo ili iweze kuwafikia watu.wengi zaidi kwa manufaa yetu na wananchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo ,Levina Lemomo akizungumza kwa niaba ya washiriki hao amesema kuwa,elimu hiyo ataitumia vizuri katika kuhakikisha jamii.inakuwa na uelewa mpana wa kutosha kuhusu mkondo huo kwani una manufaa makubwa sana katika.nchi yetu.
Kauli mbiu ya mafunzo hayo yaliyoshirikisha wathibiti ubora wa halmashauri 184 ni “Utoaji wa elimu bora ya Amali hutokana na tathmini makini ya ujifunzaji na ufundishaji.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na wadau wa maendeleo ya elimu wanaoshirikiana na serikali ya awamu ya sita kupitia miradi mbalimbali katika kuboresha elimu ukiwemo “mradi wa uimarishaji wa ubora wa elimu ya sekondari (SEQUIP)kwa kufadhili mafunzo haya muhimu ambayo yanatekeleza matakwa ya mtaala ulioboreshwa.