Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 02.12.2024 ilitoa elimu juu ya madhara ya usafirishaji haramu wa dawa za kulevya kwa madereva zaidi ya 48 wa magari madogo (_Noah_) yanayobeba abiria kutokea Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha kuelekea Mpaka wa OSBP Namanga wilayani Longido Arusha (M).
Madereva hao waliaswa kutokujihusisha na matumizi pamoja na usafirishaji wa dawa za kulevya kwani vitendo hivyo vinaweza kupelekea kufungwa jela maisha pamoja na vyombo vyao vilivyotumika kusafirishia dawa hizo kutaifishwa na kuwa mali ya umma.
Pia, walihamasishwa kuwa mabalozi wazuri wa kupiga vita dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wasafirishaji haramu wa dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya Mamlaka ya 119.