Naibu Waziri wa fedha Othman Chande ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha Dkt.Mwingulu Nchemba akizungumza  katika mahafali ya 84  ya wachungaji katika chuo cha International Evangelism Church kilichopo Sakila mkoani Arusha.
Askofu wa makanisa ya International Evangelism Church Tanzania,Dkt Eliud Issagya akizungumza katika mahafali hayo mkoani Arusha .
…………
Happy Lazaro, Arusha .

Wahitimu   wa Chuo cha biblia Sakila wametakiwa  kutumia nafasi zao vizuri katika kukemea  swala la maadili na malezi katika maeneo yao sambamba na kuacha tamaa kwani huo ndio  msingi ulio bora.

Hayo yamesemwa na  leo  na Naibu Waziri wa fedha Othman Chande ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha Dkt.Mwingulu Nchemba katika mahafali ya 84  ya wachungaji katika chuo cha International Evangelism Church kilichopo Sakila mkoani Arusha ambapo jumla ya wahitimu 73 wamehitimu kozi ya biblia  chuoni hapo.
Chande amesema kuwa, endapo wachungaji watatumia nafasi zao ipasavyo itasaidia sana kupunguza maovu mbalimbali.katika.jamii ikiwa ni pamoja na  kuhubiri amani katika jamii.
“Nawaombeni  sana muepukane na rushwa  katika kazi zenu kwani ndio inapelekea  kuwa na tamaa na kusababisha watu kutoka kwenye msingi ya maadili badala yake nyie mkawe  mstari wa mbele na mabalozi katika kukataa na kukemea rushwa “amesema .
“Baba Askofu nakupongeza  sana kwa kitendo ulichofanya cha kuanzisha chuo hiki kwani ni jambo kubwa sana na kwa kufanya hivyo umelitendea  haki  neno la Mungu .’amesema
Aidha Chande amewataka wachungaji kuhubiri haki katika maeneo yao na wawe na mapenzi ya dhati na wasiwe na tofauti na wenzao badala yake waendelee kupendana  na kutenda  haki  kwa kila mmoja .
Chande amewataka kutumia nafasi zao vizuri katika kuepuka wivu,choyo na husda kwani.hizo ndizo zina madhara makubwa katika.maisha  ya mwanadamu .
“Serikali inatambua kwa kiwango kikubwa sana mchango wa  taasisi za dini kwani zinafanya kazi nzuri sana ya kusaidia serikali na sisi tupo pamoja katika kuhakikisha malengo yao yote yanafikiwa.,
“amesema Chande .
Naye Askofu wa makanisa ya International Evangelism Church Tanzania,Dkt Eliud Issagya amesema kuwa, chuo hicho kina miaka 41 sasa tangu kuanzishwa kwake ambapo kimekuwa kikitoa  kozi ya uchungaji. 
Amesema kuwa,wao kama viongozi wa dini wamekuwa  wakishirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kwani zimekuwa zikiharibu  vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Askofu Dkt.Issagya amewataka wahitimu hao kuendeleza vipaji vyao walivyopata  katika kuisaidia  jamii katika maswala mbalimbali ikiwemo kuhubiri  amani na upendo katika jamii inayowazunguka. 
Naye Mmoja wa wahitimu akisoma  risala, Richard Meru  amesema kuwa mbali.na masomo.ya biblia chuo hicho kimeweza  kutoa  elimu kuhusu kazi za mikono na kuweza kuwaandaa kuwa wachungaji wazuri ambao watahudumia jamii katika nyanja mbalimbali .