Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Bwana Chagu Nghoma akizungumza na Wanahabari wakati wa hafla ya kuupokea Mradi wa kusambaza majiko ya gesi katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza, tarehe 3 Desemba, 2024.
…….
📌Kila wilaya kusambaziwa majiko 3,255
📌Shilingi milioni 409 kutumika kwa ajili utekelezaji wa kazi hiyo
Mkoa wa Mwanza unataraji kupokea majiko ya gezi ya kilo 6; kupitia Mradi wa kusambaza nishati ya kupikia, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo jumla ya shilingi milioni 409.15 zimetengwa kwa kazi hiyo.
Hayo yamesemwa, Tarehe 3 Disemba, 2024 na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Bwana, Chagu Nghoma baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA katika mkoa huo iliyowasilishwa na Mhandisi Mwandamizi wa Miradi, Deusdedith Malulu, katika ofisi za Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza.
“Nawapongeza REA kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, nishati hii ni salama na rafiki katika utunzaji wa mazingira pamoja na kuteletea Miradi mbambali ya nishati katika mkoa wetu, ikiwemo fursa ya ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta maeneo ya vijijini, pamoja ruzuku kwenye mifumo ya umeme jua” Amesema, Bwana Chagu.
“Kwa ujumla, Mwanza ni mkoa wenye visiwa vingi, ambavyo kupata umeme wa grid ya taifa ni kazi ngumu, tunamshukuru, Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan; Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa kutoa kipaumbele kwa maeneo ya visiwani, mfano Ukerewe ina visiwa 38. Mradi wa umeme jua utasaidia Wananchi wengi kupata nishati ya umeme”. Alisema Bwana Chagu
Aidha, Bwana Chagu ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Mwanza kuchangamkia fursa ya Miradi yote iliyoletwa na REA kwa mkoa huo na ameahidi kutoa ushirikiano na kuwahamasisha Wananchi kununua majiko hayo ya gesi kwa nusu bei.
Kwa upande wake, Mhandisi Malulu amezitaja wilaya zinazonufaika na Mradi majiko ya gesi, kuwa ni pamoja na wilaya ya Kwimba, Misungwi, Magu, Sengerema, Buchosa na Ukerewe.
“Kila wilaya itasambaziwa majiko ya gesi 3,255 kupitia kampuni ya LAKE Gas Limited. Tunaendelea kuhamasisha kujitokeza kwa wingi kuchukua mitungi hii inayotolewa kwa bei ya punguzo ya asilimia 50.” Amesema, Mhandisi, Malulu.
Ameongeza kuwa, elimu ya matumizi sahihi ya nishati safi itaendelea kutolewa kwa Watanzania ili kuhamasisha na kuchochea jamii kutumia nishati safi na salama ya kupikia.
Wakati huo huo, Mhandisi Malulu amemueleza Mkuu wa mkoa Geita kuwa REA imeleta fursa ya mkopo na nufuu wa ujenzi wa vituo vidogo vya bidhaa za mafuta vijijini yaani (Diseli na Petroli) ambapo kila Mwananchi mwenye nia ya kutaka kujenga kituo kidogo cha mafuta vijijini anaweza kuomba mkopo wenye riba nafuu pamoja na ukomo wa miaka saba na kuongeza kuwa shilingi milioni 133 zinakopeshwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo kimoja cha mafuta.
Mhandisi Malulu ameongeza kuwa masharti ya kupata mkopo huo ni nafuu na kwamba masharti ya mkopo huo pamoja fomu za maombi, zinapatikana kwenye tovuti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa anwani ya (www.rea.go.tz)
Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Bwana Chagu Nghoma akizungumza na Wanahabari wakati wa hafla ya kuupokea Mradi wa kusambaza majiko ya gesi katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza, tarehe 3 Desemba, 2024.
Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Bwana Chagu Nghoma akizungumza na Wanahabari wakati wa hafla hiyo.
Mhandisi Mwandamizi wa Miradi, kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bwana Deusdedith Malulu, akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Miradi mbambali inayotekelezwa na REA mkoani Mwanza mbele ya Wanahabari katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza hivi karibuni.
Mhandisi Mwandamizi wa Miradi, kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bwana Deusdedith Malulu, akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Miradi mbambali inayotekelezwa na REA mkoani Mwanza.