Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Everwell Cable kinachotengeneza Nyaya za umeme na Nguzo za zege kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Disemba 03,2024.
….
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo amewataka wawekezaji Nchini kuongeza wigo wa uwekezaji nchini ili kuendeleza uchumi wa Viwanda Nchini.
Amesema wamiliki wa Viwanda wana haja kubwa ya kuitana Nchini pamoja na kuongeza wigo wa uwekezaji wa Viwanda kwenye maeneo mbalimbali yaliyopo nchini.
Dkt.Jafo amebainisha hayo alipotembelea Kiwanda cha Vioo cha KEDA kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani Disemba 03,2024.
Aidha Waziri Jafo ameridhishwa na shughuli za uzalishaji zinazofanywa na Kiwanda hicho ambacho kina soko kubwa la vioo ndani na nje ya Nchi ya Tanzania kuwa moja ya Kiwanda kilichotoa ajira kwa watu 800 ambapo ni matumaini yake mpaka kukamilika kwa kiwanda hicho kutaweza kutoa ajira zaidi ya watu 3000 ambapo itakuwa fursa kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Katika ziara yake hiyo Waziri Jafo pia ametembelea kiwanda cha Everwell Cable kinachotengeneza vifaa vya umeme ikiwemo Nyaya na Nguzo za zege.
Katika Kiwanda hicho Dkt.Jafo ameagiza Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya uwekezaji wa Viwanda ikiwa ni Mpango mahsusi wa Wizara wa kuhakikisha kila Mkoa na Halmashauri kuna kuwa na Viwanda mbalimbali.
Waziri Jafo pia amesema Wizara ya Viwanda na Biashara imeamua kujikita na ajenda hiyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuweka mazingira wezeshi na rafiki ili kuvutia wawekezaji wote wanaofika nchini,kujenga uchumi pamoja na kuhakikisha Serikali inapunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana kwenye kila Mkoa na Halmashauri zote na Taifa kwa ujumla.
Amesema Wizara ipo katika kusaidia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ya uwekezaji wa Viwanda nchini yanatimia na ndio maana Wizara imekuja na Mpango wa ujenzi wa Viwanda wa Miaka Sita katika Mikoa na Wilaya zote Nchini.
Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Bw. Omary Mwanga akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo amesema uwekezaji wa viwanda hivyo umekuwa msaada mkubwa kwenye ajira kwa vijana,Mapato ya Serikali lakini pia kushirikiana kwenye mambo ya kijamii.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) akitembelea Kiwanda cha Vioo cha KEDA ili kuona shughuli za uzalishaji wa Vioo katika kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) akitembelea Kiwanda cha Everwell Cable kinachotengeneza Nyaya za umeme na Nguzo za zege kuona shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) akipewa maelezo mafupi na Mkurugenzi Msaidizi wa kiwanda cha Everwell Cable kinachotengeneza Nyaya za umeme na Nguzo za zege Bw. Chang, kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Everwell Cable kinachotengeneza Nyaya za umeme na Nguzo za zege kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Disemba 03,2024.