Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipowasili nyumbani kwa marehemu Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Novemba 2024.
……
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema marehemu Dkt. Faustine Ndugulile alikua kiongozi mwenye nidhamu, rafiki wa kila mtu na kiongozi aliyeweza kutetea vema maslahi ya Taifa.
Makamu wa Rais amesema hayo alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndugulile Kigamboni Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuifariji familia pamoja na waombolezaji wote.
Makamu wa Rais amewaombea faraja na moyo wa uvumilivu wote walioguswa na msiba huo. Amewashukuru wote walioshiriki katika kuifariji familia wakati huu wa kipindi kigumu kwao na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kushirikiana katika nyakati mbalimbali zinazojitokeza katika jamii ikiwemo za majozi na furaha.
Aidha amesema inapaswa kuendelea kumshukuru Mungu kwa maisha ya Dkt. Ndugulile hapa duniani. Ameongeza kwamba ni vema kwa Watanzania kuendelea kuishi vizuri na ndugu na majirani.
Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amesali pamoja na familia, ndugu, jamaa na marafiki kumuombea marehemu Dkt. Faustine Ndugulile.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na waombolezaji mbalimbali wakati akiwasili nyumbani kwa marehemu Dkt. Faustine Ndugulile Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Novemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipowasili nyumbani kwa marehemu Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Novemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisali pamoja na mjane wa marehemu Dkt. Faustine Ndugulile, Dkt. Magdalena Lyimo, watoto pamoja na wana familia wengine wakati alipofika kuwafariji Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Novemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji mbalimbali wakati alipowasili nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika marehemu Dkt. Faustine Ndugulile Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Novemba 2024.