Kampuni ya Dhahabu ya Barrick (NYSE:GOLD)(TSX:ABX) imepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Ontario wa kutupilia mbali madai yaliyotolewa na wakazi wa Tanzania waliokuwa wakilalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania jirani na mgodi wa dhahabu wa kampuni hiyo wa North Mara.
Mahakama hiyo iliamua kwamba Ontario haikuwa jukwaa mwafaka la kusikiliza madai hayo.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, alisema kampuni hiyo imekanusha mara kwa mara kile inachokiona kama madai yasiyo na msingi yanayotolewa asasi chache zisizo za serikali zenye mrengo wa kianaharakati zinaodai kuwapo kwa ukiukwaji wa kihistoria wa haki za binadamu katika maeneo yanayozunguka mgodi wake wa North Mara.
“Tunajivunia mafanikio tuliyoyapata nchini Tanzania kutokana na ushirikiano wetu na Serikali ya nchi hiyo kupitia ubia wa Twiga. Mchango wa mapato ya migodi yetu umeleta mageuzi katika uchumi wa nchi hiyo wakati uwekezaji wetu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jamii za wenyeji, ukiambatana na mkakati wetu wa kuleta maendelea ya jumla, umeboresha hali ya maisha yao,” alisema.