Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora na Fursa cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Salvator Mbilinyi amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti.
Kupitia kikao hicho kilichofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba viongozi hao wamejadili mbinu za
kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na IOM katika kuhamasisha mchango wa
diaspora kwenye maendeleo ya Taifa.
Mazungumzo hayo pia yalihusisha mipango na mikakati ya kuendesha zoezi la kubaini utambuzi na usambaaji wa diaspora wa Tanzania duniani ili kujua idadi yao duniani, kuelewa demografia na ujuzi wao.
Hatua hii itawezesha utekelezaji wa mikakati kwa kutumia taarifa za ujuzi na rasilimali watu muhimu kuwezesha maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
Kikao hicho ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuhakikisha diaspora wanakuwa washirika muhimu wa kukuza ustawi wa Taifa kupitia mipango kabambe inayozingatia na kuthamini michango ya diaspora inayowezesha maendeleo endelevu
ya Taifa.
#DiasporaMapping #TanzaniaDiaspora #IOM #MaendeleoYaTaifa