Wahitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’
Wahitimu wa mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom wakipokea keki kwa niaba ya wahitimu wengine.
Na Mwandishi wetu – Malunde 1 blog
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Samson Hango, ameongoza sherehe za mahafali ya 16 ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2024 katika Shule ya Sekondari Kom ‘Kom Secondary’, iliyopo katika eneo la Butengwa, Manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 131 walihitimu elimu ya Kidato cha Nne
Mahafali hayo yamefanyika leo, Jumamosi, Novemba 23, 2024, katika viwanja vya shule ya Kom yakihudhuriwa na mamia ya wazazi, wageni waalikwa, wanafunzi, na watu mbalimbali wenye mapenzi mema kwa shule hiyo ikiwa ni sherehe ya kipekee inayosherehekea mafanikio ya wanafunzi hao waliomaliza kidato cha nne kwa mwaka huu.
Akizungumza wakati wa Mahafali,Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawalipia ada watoto wao kwa wakati ili kuondoa vikwazo katika mchakato wa elimu.
Amesisitiza kwamba, elimu ni gharama, na hata shule za serikali (public schools) zina gharama zake, ikiwemo michango ya wananchi.
“Nimeambiwa kuna baadhi ya wazazi wanachelewa kulipa ada.Niwakumbushe tu kuwa ukimpeleka mtoto katika shule binafsi nivvizuri kuhakikisha unalipa ada,. Elimu ni gharama, hata kwenye shule za serikali ‘ Public Schools’ kuna gharama,kuna nguvu za wananchi wanachangia pia”,amesema Hango.
Aidha, Hango amekumbusha wazazi kuwa ni muhimu kumpeleka mtoto shule mara tu inapofunguliwa ili kumhakikishia mafanikio katika masomo.
“Ni muhimu kumpeleka shule mtoto mara tu shule inapofunguliwa,kwani shule ikifunguliwa masomo yanaanza. Usimuweke mtoto nyumbani, anafanya nini nyumbani muda wa shule?,amehoji Hango.
Amewasihi wazazi kuwakatia bima ya afya watoto wao ili kuhakikisha wanapata matibabu pindi wanapohitaji.
Aidha Hango ameipongeza Shule ya Sekondari Kom kwa juhudi zake za kujitahidi kielimu na kinidhamu, ikionyesha mafanikio makubwa katika mitihani ya mkoa na taifa.
Naye Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom , Jackton Koyi ametumia fursa hiyo kumshukuru serikali kwa msaada wake katika kufanikisha malengo ya shule, akitaja kuwa Kom imekuwa daraja muhimu kwa wanafunzi wengi wanaoendelea na masomo katika vyuo vikuu na shule za kidato cha tano.
Amesema shule hiyo na aamewahimiza wazazi kuendelea kuleta watoto wao katika shule hiyo.
“Naomba wazazi muendelee kutuamini na kuleta wanafunzi katika shule hii ambayo iimeendelea kufanya vizuri kitaaluma”,ameeleza Koyi.
Koyi ameongeza kuwa shule ya Kom pia ina shule ya awali na shule ya msingi, ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika kutoa elimu bora kwa jamii.
“Licha ya shule ya sekondari Kom, pia tuna shule ya awali na shule ya msingi Kom iliyoanzishwa mwaka 2016 ipo nyuma ya ofisi za KASHWASA umbali wa takribani mita 500 kutoka shule ya sekondari Kom”,amesema.
Awali akisoma taarifa ya shule mkuu wa shule ya sekondari Kom Grace Mutabilwa amesema mwaka huu, idadi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne ni 131, akionyesha mafanikio ya shule hiyo katika kutoa elimu bora.
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango (kushoto) akiwa katika mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom, Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi – Picha Malunde Media
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango (kushoto) akiwa katika mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom, Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi akitoa neno la salamu wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi akitoa neno la salamu wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akizungumza na wazazi na walezi katika sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi .
Mkuu wa shule ya Sekondari Kom, Grace Mutabilwa akitoa taarifa ya shule wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Wahitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom
Wahitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom Wahitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom
Mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom.
Wahitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya Sekondari Kom wakisoma Risala.
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akiwatunuku vyeti wahitimu mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akiwatunuku vyeti wahitimu katika sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akiwatunuku vyeti wahitimu katika sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akiwatunuku vyeti wahitimu katika sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akiwatunuku vyeti wahitimu katika sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi
Walimu wa shule ya Sekondari Kom,wakiburudika wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Meneja wa shule ya Sekondari Kom, Magreth Koyi akicheza ngoma za asili wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Walimu wakishangilia baada ya kupokea keki kutoka kwa whitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya Sekondari Kom.
Burudani zikiendelea katika mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom