Wadau, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wajasiriamali, familia na wananchi wote wamekaribishwa kushiriki sherehe za Ilemela Nyama Choma zinazofanyika kila jumamosi ya wiki katika viwanja vya Nane nane Nyamhongolo ili kuburudika na kujikwamua kiuchumi
Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa sherehe hizo Ndugu Emanuel Juma wakati wa muendelezo wa sherehe hizo katika viwanja vya Nane nane Nyamhongolo kwa wiki ya pili baada ya kuzinduliwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe Said Mtanda ambapo amewaomba wananchi kutumia fursa hiyo kwaajili ya kujiendeleza kiuchumi pamoja na kutumia sherehe hizo kama sehemu ya burudani na kuondoa msongo wa mawazo
‘.. Shughuli hizi za uchomaji nyama zilizindukiwa rasmi wiki iliyopita na mkuu wa mkoa wetu, Kikubwa nawaomba wananchi wa Ilemela na mkoa wa Mwanza kwa ujumla kutumia vyema uwepo wa sherehe hizi kama sehemu ya kuinua uchumi wao na kustareheka na familia zao ..’ Alisema
Aidha Ndugu Emanuel ameongeza kuwa wafanyabiashara ambao mpaka sasa bado hawajajitokeza kushiriki shughuli hizo bado nafasi ipo na wanakaribishwa kushiriki
Zephania John ni mfanyabiashara kupitia kampuni ya Harvard Foods Swahili Flavor ambapo amepongeza uwepo wa sherehe hizo Kila mwisho wa wiki kwani zinatoa nafasi kwa wananchi kujumuika pamoja na kuburudika huku mazingira yakiwa rafiki Kwa rika zote na jinsia zote
Akihitimisha Bwana Tito Deo kutoka kampuni ya City Center ameipongeza manispaa ya Ilemela kwa kubuni sherehe hizo huku akitamani uwepo wa nyama pori katika eneo hilo ili kutoa fursa kwa wananchi kupata ladha mpya ya vyakula na vinywaji ambavyo wengi hawajavizoea
Ilemela Nyama Choma inafanyika kila jumamosi ya wiki kuanzia saa mbili asubuhi mpaka usiku ikipambwa na vinywaji, vyakula,mziki na burudani