Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa Pallangyo akizungumza wakati akitoa taarifa kwenye Mahafali ya 22 ya taasisi hiyo Kampasi ya Singida yaliyofanyika jana Novemba 22, 2024.
Na
Mwandishi Wetu, Singida
TAASISI
ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida imefanya jumla ya tafiti 15 na
kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa
taasisi hiyo, Profesa William Pallangyo wakati akitoa taarifa kwenye Mahafali
ya 22 ya taasisi hiyo Kamapasi ya Singida Novemba 22, 2024 ambayo yaliwahusisha
wahitimu 1,477 wa Kampasi ya
Singida, wakiwemo wanawake 812 (sawa
na asilimia 55) na wanaume 665 (sawa
na asilimia 45).idadi ambayo ni sawa na asilimia 13 ya wahitimu wote 11,620
wa kampasi za Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma na Singida, kwa
Mwaka wa Masomo 2023/2024.
Pallangyo alisema wahitimu hao waliotunukiwa Cheti cha Awali
walikuwa ni 399, Cheti 447, Stashahada 443, na Shahada 188 katika fani mbalimbali kuwa mahafali hayo
yalifanyika sambamba na uzinduzi wa program ya shahada ya uzamili uzinduzi
ulifanywa na mgeni rami Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.
Alisema
ili kuendeleza na kutimiza malengo ya Taasisi, Kampasi ya Singida imeendelea
kufanya tafiti zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, hususan
katika maeneo ya Uhasibu na Fedha, Ununuzi na Ugavi, Rasilimali Watu, Maktaba,
na Ujasiriamali.
“ TIA inaendelea kuboresha miundombinu
ili kuhakikisha ongezeko la wanachuo linakwenda sambamba na ubora wa huduma na
kueleza kuwa Kampasi ya Singida imepokea kiasi cha Sh. za Kitanzania Bilioni 13.5
kupitia Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Vyuo vya Elimu ya Juu na kuwa fedha
hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Taaluma.
Alisema jingo hilo litakuwa
na vyumba vya madarasa, kumbi za mihadhara, ofisi, vyoo maalumu kwa watu wenye
mahitaji maalum, na chumba cha kunyonyeshea na kuwa litakapo kamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo 3,637
kwa wakati mmoja.
“Nitumie fursa hii
kuishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwezesha kupatikana kwa fedha hizo,
ambazo ni mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Dunia,” alisema Pallangyo.
Profesa Pallangyo aliongeza kuwa katika
kuhamasisha shughuli za kijamii na kukuza uhusiano na jamii inayowazunguka,
Kampasi ya Singida imeanzisha mpango mkakati wa miaka minne (2023-2027) wa
kuboresha somo la Hisabati katika shule za sekondari za Singida mpango unaoendeshwa
na Mhadhiri Msaidizi Mary Kayanda na kuwa kwa sasa unatekelezwa katika Shule
ya Sekondari Mandewa.
Alisema TIA kupitia Kampasi
ya Singida inaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuendelea kuimarisha
sekta ya elimu na uchumi kupitia mafunzo, utafiti na ushauri wa kitaalam.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Halima Dendego ambaye alikuwa
mgeni rasmi akihutubia kwenye mahafali hayo aliwasihi
wahitimu hao kutumia
mitandao ya kijamii kama jukwaa la kutangaza bunifu zao, kukutana na wateja na
kueneza mawazo mapya badala ya kupoteza muda mitandaoni kwa mambo yasiyokuwa na
manufaa.
“ Mitandao hii inatoa fursa kubwa ya
kujitangaza, kukuza biashara, na kufikia mafanikio makubwa ya mtu mmoja mmoja
na taifa kwa ujumla,” alisema Dendego.
Dendego aliwakumbusha wahitimu hao kwamba, taswira ya Chuo hicho imejengwa na
wahitimu waliowatangulia hivyo popote watakapokuwa hasa kwa wale watakaosoma
vyuo vingine wakafanye bidii ili vyuo hivyo viweze kuendelea na kuvutiwa na
wahitimu hao kutoka TIA na kwa wale watakaobahatika kufanya kazi basi wakafanye
kazi kwa umahiri na maadili ili kuendeleza taswira nzuri ya TIA.Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia kwenye mahafali hayo.
Wahadhiri wa TIA Kampasi ya Singida wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa sehemu Ukuzaji na Uendelezaji wa Wanafunzi Kitaaluma na Kitaalamu, Imani Matonya (kushoto) akielezea kazi mbalimbali za ubunifu zinazofanywa na Wanafunzi wa taasisi hiyo wakati mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego alipotembelea banda la wabunifu hao kuona kazi zao.
Wahitimu wakitunukiwa vyeti vyao kwenye mahafali hayo.