Na Mwandishi Wetu – Rukwa
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma a Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Kwela, Mhe.Deus Sangu amewataka wananchi wasisahau maendeleo wanayoyaona katika Jimbo la hilo ni kutokana na jitihada za Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni za Serikali za Mitaa uliofanyika katika Kjiji cha Ilemba, Kata ya Kalambanzite katika Jimbo la Kwela Mkoani Rukwa.
Amefafanua kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Kata ya Kalambanzite imeimarika katika sekta ya afya, elimu, barabara, maji pamoja na umeme.
Amewataka wananchi hao kujitokeza ifikapo Novemba 27 mwaka huu ili kuchagua viongozi wenye maono na mwelekeo wa kuwaunganisha kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa ambao ni Wagombea kupitia CCM.
” Chagueni viongozi ambao wana uelewa wa matatizo na kujua namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi pasipo kujali rangi, kabila au eneo” amesema Mhe.Sangu
Mhe.Sangu amewaeleza Wanachi wa Kata hiyo ya Kalambanzite kuwa wana kila sababu ya kuchagua Chama chenye Sera zinazotekelezeka ambacho ni Chama Cha Mapinduzi na kuachana na vyama vingine ambavyo sera zao zimelenga kuhubiri chuki na utengano.
“ Nimekuja kuwaomba mtuunge mkono kwa kupiga kura na kuchukua vijiji na vitongoji vyote” ameomba Mhe.Sangu
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa, Patrick Maufi amewashukuru wagombea waliopitishwa na kusema hadi sasa CCM imesimamisha wagombea bila kupingwa katika ngazi mbalimbali katika uchaguzi huu.
Hata hivyo Mjumbe huyo amewataka Wananchi wakapige kura ya ndiyo kwa baadhi ya wagombea waliopita bila kupingwa.