NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewahimiza wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi wote kwa ujuma kuhakikisha kwa hawafanyi makosa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuhakikisha wanakwenda kuwachagua wagombea wote wa CCM lengo ikiwa ni kushinda kwa kishindo katika mitaa yote 73.
Koka ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kampuni za chama cha mapinduzi (CCM) Kata ya Kongowe zilizofanyika katika eneo la Bamba na kuhudhuliwa na wanachama wa chama hicho pamoja na wakiwemo wananchi pamoja naa viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jumuiya zake.
Koka amesema kwamba wakichaguliwa viongozi wote wa CCM inatoa urahisi wa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na kupanga mambo ya maendeleo kwa pamoja tofauti na kuchanganya na vyama vingine.
“Ndugu zangu mimi Mbunge wenu leo nimekuja kwa ajili ya kuwazindulia rasmi kampeni hizi za uchaguzi na mimi kitu kikubwaambacho ninawaomba ni kunichagulia wagombea wote wa chama cha mapinduzi ambao na mimi nitafanyanao kazi begaa kwa bega na hii ni katika kumsaidia Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutimiza wajibu wake wa kuwaletea maendeleo wananchi,”alisema Koka.
Amesema kwamba kwa sasa Jimbo la Kibaha limeweza kuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ambayo yameatokana naa juhudi zake kwa kushirikiana na wenyeviti ambao wamemaliza muda wao lakini ana imani katika uchaguzi huu wagombea wote ambao wameeteuliwa wataweza kuendelea kuwahudumia wananchi ikiwemo kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Koka amemshukuru Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kusaidia katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kimkakati sambambaa na kuweza kujenga shule mpya katika jimbo lake ambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha ufaulu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kongowe Hamis Shomari amesema kwamba wagombea ambao wameteuliwa kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya chama wanamatarajio makubwa ya kuibuka naa ushindi katika uchaguzi huo kutokana na kuwa na uwezo na sifa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Diwani huyo amesema kwamba kutokana na chama cha mapinduzi kilivyojipanga kuanzia ngazi zote watahakikisha kwamba wanashinda katika mitaa yote na kuwapata viongozi ambao atakwenda kufanya nao kazi ya pamoja katika suala zima la kuwaletea maendeleo ikiwemo sektaa yaa elimu, afya, maji pamoja na miundombinu ya barabara, sambamba na huduma nyingine za kijamii.
Nao baadhi ya wagombea katika nafasi ya uenyekiti akiwemo Nuru Awadhi amesema kuwa wamejiandaa vema katika uchaguzi huo na kuahidi endapo wakichaguliwa katika uchaguzi huo wataweza kushirikiana na wananchi katika kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi na kuwaletea maendeleo.