Na Prisca Libaga Tanga
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 20.11.2024 imetoa elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa Maafisa Udhibiti wa Mpaka wa OSBP Horohoro, Wafanyabiashara na Wananchi wa Mpaka wa OSBP Horohoro pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Duga wilayani Mkinga Mkoa wa Tanga.
Zaidi ya washiriki 710 walipatiwa elimu hiyo. Walihamasishwa kushirikiana na Mamlaka katika udhibiti na mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo katika eneo la mpakani kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.