Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dkt. Elikana John wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaofanyika Baku, Azerbaijan.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia wasilisho la Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dkt. Elikana John (hayupo pichani) kwenye mkutano wa pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaofanyika Baku, Azerbaijan.
….
TANZANIA imetoa wito kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuunganisha mifumo ya teknolojia katika ufuatiliaji na usafirishaji wa mazao ya misitu ili kupunguza tatizo la uvunaji na usafirishaji haramu.
Pia, inatarajia kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) ili kuongeza juhudi katika upatikanaji wa rasilimali fedha na teknolojia za ufuatliajia wa mazao ya misitu kuanzia kwenye maeneo yanapovunwa
Wito huo umetolewa Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dkt. Elikana John wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaofanyika Baku, Azerbaijan.
Mkutano huo umelenga kuangalia mchango wa sekta ya misitu kwenye kupunguza uzalishaji wa gesi joto katika ufuatiliaji na usimamizi endelevu wa misitu barani Afrika.
Aidha, mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu (MECCF) ya Kenya, Wakala wa Misitu Kenya (KFS) na JICA.
Dkt Elikana alifanya wasilisho pamoja na wadau wa Afrika ya Mashiriki kuhusu matumizi ya teknolojia na mifumo ya kufuatilia usafirishaji wa mazao ya misitu unayofanywa na TFS ili kuendeleza uvunaji endelevu na kuimarisha uhifadhi wa misitu na kupunguza uvunaji haramu, lakini pia kuongeza mapato ya Serikali,
Mkutano huu umewaleta pamoja na kuwaunganisha wadau wa Afrika mashariki, washirika wa maendeleo wakiongozwa na JICA katika kuchagiza na kujenga uelewa wa wadau na kuwezesha utalaam na upatikanaji Rasilimali Fedha kwa wadau wa Afrika Mashariki.