Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amezindua Rasmi zoezi la utoaji wa Mikopo ya Asilimia 10 kwa Vikundi vya Wanawake , Vijana na Watu wenye ulemavu , ambazo ni Fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri na kutoa Hundi ya Mfano yenye thamani ya Shilingi Milioni 817,619,365.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu tarehe 18 Novemba katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi ( Ifakara FDC) uliopo uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara
” Nawapongeza sana Vikundi vyote , Fedha hizo mkazitumie kulingana na Malengo mliyojiwekea . Halmashauri inaenda kutoa Fedha Milioni 817, 619,365 kwa makundi matatu , Wanawake , Vijana na Watu wenye Ulemavu, mkazitumie vizuri Ili mkatimize Malengo yenu” . Alisema Mhe. Kyobya
Wakati huohuo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bibi. Witness Kimoleta aliwasihi wote walioomba na watakaopata Mikopo hiyo kuzingatia kanuni, taratibu na Sheria za Mikopo ili ikatoe matokeo chanya katika shughuli wanazoenda kuzifanya na kutimiza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha makundi mbalimbali ya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu yanajikwamua kiuchumi.
” Tumewaandaa Maafisa wanaoshughulikia Mikopo kuendelea kutoa Elimu na kuwatembelea mara kwa mara katika maeneo yao kuhakikisha shughuli wanazofanya zinaleta tija”. Alisisitiza Bibi. Kimoleta na kuongeza
” Kiasi cha Sh. Milioni 261,000,000 kitatolewa kwa Kata 15 kati ya 19 kwa Vikundi vilivyokaguliwa na kukidhi vigezo kwa awamu ya kwanza , awamu nyingine zinafuatia, Halmashauri ya Mji Ifakara iko bega kwa bega na Wananchi kuhakikisha kwamba wanatumia Mikopo vizuri na Mikopo hiyo inaleta Mabadiliko katika maisha yao”. Alimaliza Bi. Kimoleta