Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa akizungumza kwenye hafla fupi ya kupokea magari.
Magari yaliyoletwa kwaajili ya kuimarisha usalama barabara.
Baadhi ya maafisa wa Jeshi la polisi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kamanda wao baada ya kupokea magari matatu yatakayosaidia kuimarisha ulinzi
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa onyo kwa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani huku likiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Hayo yamebainishwa Leo Novemba 15,2024 wakati wa kupokea magari matatu yaliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza yatakayotumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo doria ya masafa marefu (Highway Patrol).
Akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wakati wa kupokea magari hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa amesema magari mawili GWM Pick up dable cabin yatatumika kufanya doria ya masafa marefu kwa upande wa usalama barabarani na Toyota Land Cruiser GXR Itatumika katika shughuli za kiutawala.
“Kwa madereva ambao wamekuwa wakifanya makosa ya usalama barabarani na kukimbia wakidhani hatuna uwezo wa kuwafikia sasa hivi tutawakama kirahisi keani magari haya yanaenda zaidi ya spidi mia mbili”
“Sioni dereva yeyote atakaye fanya kosa la usalama barabarani na asiweze kukamatwa na askari hivyo wakae chonjo na wabadilishe mienendo na tabia zao” amesema Kamanda Mutafugwa.
Katika hatua nyingine Kamanda Mutafugwa amepoke viti 150 vya plastiki vilivyotolewa na kampuni ya JEMA kwa ajili ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi za kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi.