Na.Alex Sonna-DODOMA
Mkuu wa Wizara ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri ameshiriki mazoezi na watumishi wa Wizara ya Afya na kuwashauri watumishi kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza mara baada ya kushirikia mazoezo hayo yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Madhimisho ya Wiki ya Kuzuia Magonjwa yasiyoambukiza matembezi yaliyoanzia uwanja wa Jamhuri na kumalizikia viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Shekimweri amewashauri watumishi wa Wizara hiyo kujenga timu imara ya mazoezi na ikiwezekana kutenga siku ya kufanya mazoezi hata muda mchache wa kufanya mazoezi.
“Katika maadhimisho haya nawaomba wananchi mjitokeze kupimwa afya zenu pamoja na kupewa ushauri wa Madaktaria jinsi ya kufanya mazoezi kulingana na umri utaambiwa Mazoezi gani kwa umri gani maana kuna wakati umri Umesogea lakini unataka mazoezi ya kijana wa miaka 19 utatuleta mgogoro, kijana mdogo unataka kufanya mazoezi ya kibabu pia hayatakusaidia kwenye kujenga afya yako, ” amesisitiza
Hata hivyo Shekimweri amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja kumchukua kiongozi wao anayefaa katika kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea amesema magonjwa yasiyoambukiza ya naweza kuzuilika kirahisi na bila kutumia gharama yoyote hivyo ni wajibu kila mtanzania kuamka nakufanya mazoezi.
Amesema kuwa mazoezi yaliyofanyika leo ni mwanzo wa mpango wa Wizara hiyo kufanya mazoezi mwisho wa mwezi na mwanzo wa mwezi ili kuimarisha afya ya mwili.
“Tumeamua kumuunga Mkono Mhe,Rais Samia ambaye amekuwa akisisitiza wizara kufanya mazoezi ili watumishi waweze kutekeleza majukumu yao vizuri lazima watumishi wawe na afya bora ambayo haipatikani kupitia lishe pekee bali na kuhakikisha pamoja na utekelezaji wa majukumu wanapata muda wa kufanya mazoezi na kuimarisha afya ya mwili pia yatazidi kutuweka pamoja “, amesema Dkt.Nyembea
Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza hufanyika kila mwaka mwezi Novemba nakauli mbiu ya mwaka huu ni “Zuia magonjwa yasiyoambukiza”.