Happy Lazaro,Arusha .
Zaidi ya Washiriki 100 wakiwemo maafisa wa serikali viongozi wa asasi za kiraia na wataalamu wa kupambana na ufisadi, wamekutana mkoani Arusha ili kujadili haja ya kuwepo kwa mifumo madhubuti ya kuwalinda wapiga filimbi wanaohatarishamaisha yao kufichua ufisadi.
Aidha washiriki hao wamekutana kwenye mdahalo wa Umoja wa Afrika kujadili ulinzi wa wapiga filimbi ufisadi .
Mwenyekiti wa AUABC, Seynabou Ndiaye Diakhate amesema kuwa midahalo ya Afrika dhidi ya ufisadi, imeandaliwa na Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika Dhidi ya Ufisadi (AUABC) ambapo unafanyika mkoani Arusha kwa kwa muda wa siku mbili novemba 7 na 8 ,2024.
“Mdahalo wa siku mbili, wenye mada ya “Mifumo Madhubuti ya Ulinzi kwa Wapiga Filimbi,Zana Muhimu katika Vita Dhidi ya Ufisadi,” na linalenga kuonyesha umuhimu wa wapiga filimbi katika bara la afrika.”amesema .
Amefafanua kuwa Ufisadi, ukiwa ni shughuli ya siri, huenda usiwahi kufichuliwa mpaka pale mtu atakapouweka wazi au kupiga filimbi.
Ameongeza kuwa, ,jukumu la wapiga filimbi katika kufichua ufisadi ni muhimu sana,” amesema Mwenyekiti wa AUABC, Seynabou Ndiaye Diakhate.
Katibu Mtendaji wa AUABC, Charity Hanene Nchimunya, amesema kuwa mazungumzo hayo yanatafuta kuziba pengo lililopo kwa kutambua suluhisho la vitendo, kujenga ushirikiano na kuhakikisha mifumo madhubuti ya ulinzi inaundwa.
“Mazungumzo haya hayatachambuatu hali ya sasa ya mifumo ya ulinzi kwa wapiga filimbi kote Afrika, bali pia yataunda mapendekezo yanayoweza kutekelezwa ili kuunda sheria na sera za kitaifa.
Aidha amefafanua kuwa AUABC itawasilisha matokeo na mapendekezo muhimu kwa Vyombo vya Sera vya Umoja wa Afrika kwa ajili ya marekebisho yabaadaye.
Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika Dhidi ya Ufisadi (AUABC) ni Chombo cha Umoja wa Afrika kuhamasisha hatua za kuzuia na kupambana na ufisadi miongoni mwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika.