Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Mohamed Mussa akijibu Maswali yalioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Sekta ya Elimu kwa Kipindi cha Miaka Minne (4)ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi katika Kipindi maalum ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Mohamed Mussa akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Sekta ya Elimu kwa Kipindi cha Miaka Minne (4)ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi katika Kipindi maalum ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Mohamed Mussa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Sekta ya Elimu kwa Kipindi cha Miaka Minne (4)ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi katika Kipindi maalum ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Muandishi wa Habari wa ZBC TV Muntari Ngoma akiuliza maswali kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Mohamed Mussa wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Sekta ya Elimu kwa Kipindi cha Miaka Minne (4)ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi katika Kipindi maalum ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Muandishi wa Habari wa ZBC TV Shadya Mohamed akiuliza maswali kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Mohamed Mussa wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Sekta ya Elimu kwa Kipindi cha Miaka Minne (4)ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi katika Kipindi maalum ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR).
………

Na Rahma Khamis Maelezo   28/10/2024

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mhamed Mussa amesema bajeti ya maendeleo ya elimu imeongezeka kutoka bilioni kumi na tisa mwaka 2020 hadi kufikia bilioni mia Tano kumi na nane mwaka 2024.

Ameyasema hayo katika  Ukumbi wa ZBC Mnazimoja wakati akielezea mafanikio ya sekta hiyo ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka minne ya Dkt Hussein Mwinyi

Amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na jitihada za Serikali katika kuboresha Sekta ya elimu kwa kujenga Skuli za kisasa katika maeneo yote Unguja na Pemba ili kuleta mageuzi katika sekta hiyo.

Amefahamisha kuwa ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kutoka asilimia  25 Hadi kufikia 55 kwa darasa la saba na kutoka asilimia  55 Hadi kufikia asilimia 85.6 kwa wanawanafunzi wa darasa la kumi na mbili kwa  mwaka 2023.

Amesema  jumla ya madarasa 2,773 yamejengwa na serikali kwa kipindi cha miaka minne huku madarasa mengine mapya 2,037 ikiwemo skuli 26 za gorofa na skuli za chini 53  ujenzi wake umeanza kupitia bajeti ya  mwaka wa fedha 2024-2025.

Akizungumzia suala la ajira Waziri Lela amesema kuwa Wizara imefanikiwa kuajiri walimu 73 kwa kwa upande  wa mahitaji maalum na kujenga vyuo vya Amali vitano Unguja na Pemba  ili vijana waweze kujiajiri.

Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kushirikiana na waalimu ili kujenga mustakabali mwema kwa wanafunzi wao