“Tumeona majengo mengi hatua za ujenzi zipo zaidi ya asilimia 80 na wapo ndani ya mkataba waliowekewa na tunaamini watakamilisha ndani ya muda uliopangwa, na miradi hii itaipa nguvu NHC ijiendeshe kwa tija zaidi, naipongeza Bodi kwa usimamizi mzuri wa shirika hili ambalo tunaona limefanya mageuzi makubwa yenye tija,”amesema Mhe.Vuma
Kuhusu utunzaji wa majengo, Mwenyekiti huyo amesema kuwa serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa majengo kwenye Mji huo na yapo mbioni kukamilika hivyo ni vyema kuangalia namna ya kutunza vizuri.
“Huu Mji kwasasa unang’aa na serikali imetumia mabilioni kuujenga, baada ya muda Fulani utakutana na uchakavu majengo yatakuwa hayang’ai kama yanavyong’ara kwasasa, majengo mengi ya serikali yamekuwa yakijengwa na kukamilika vizuri baada ya muda ukienda unakuta miundombinu yote ya maji, majitaka na muonekano wa jengo inakuwa ni changamoto,”amesema.
“Wanunuzi wa nyumba za NHC ambao ni mmoja mmoja hawawezi kurejesha VAT kwa sababu hawafanyi biashara, mwaka jana serikali ilifanya maamuzi mazuri sana kwa nyumba zote ambazo thamani yake haizidi Sh.Milioni 50 zinaondolewa VAT na hilo linafanyika.”
“Lakini sisi tuna kiu ya kuona kuwa walau wanunuzi wote wa nyumba waondolewe hiyo kodi kwa kuwa shirika litakuwa limelipa kodi zote za serikali zinazohitajika ili kuwafanya watanzania wamudu kulipa fedha zinazohitajika kwenye ununuzi wa nyumba,”amesema Bw.Abdallah
Aidha, amesema kuwa kwasasa serikali imefanya vizuri kwenye sekta ya kilimo ambapo mikopo yao ni kwa riba ndogo na kupendekeza kamati iishauri serikali kuangalia namna ya kuwawezesha watanzania wanaochukua mikopo ya nyumba wapate kwa riba ndogo.
“Haya yote tumewasilisha kwa kamati wameyabeba kwa kuwa mengine ni ya kisera ili kuangalia ni kwa kiwango gani riba zitapungua ili watanzania waondokane na upangaji waingie kwenye umiliki wa nyumba,”amesema