Mkurugenzi wa Ufundi wa RUWASA Makao Makuu, Mhandisi Mariam Majala akiwa amepanda kwenye moja ya Pikipiki nane zilizotolewa kwa CBWSO Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Katika hatua ya kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira katika maeneo ya vijijini, Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Makao Makuu, Mhandisi Mariam Majala, amekabidhi jumla ya pikipiki nane kwa Vyombo vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO).
Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo, Oktoba 16, 2024, kwenye Ofisi ya Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka RUWASA na CBWSO, ikiwa ni ishara ya kujitolea na kuimarisha utendaji kazi wa vyombo hivyo ambavyo vinahusika na usambazaji wa huduma za maji kwa jamii.
CBWSO saba zilizonufaika ni Mwanya, Nyabuki na Chui zilizopo katika Wilaya ya Kahama, Nyahembe iliyopo katika wilaya ya Shinyanga na Songambele, Unyashagi na Mwandoshimba zilizopo katika wilaya ya Kishapu.
Mhandisi Majala amewapongeza RUWASA na CBWSO Mkoa wa Shinyanga kwa juhudi zao kubwa zinazofanyika katika kuhakikisha huduma za maji safi na salama zinawafikia wananchi wa vijijini.
“Tuna CBWSO nyingi nchini, lakini nyinyi mnafanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi. Leo tunafanya tukio la kihistoria kwa kuwapatia pikipiki ambazo mmezinunua kwa mapato yenu wenyewe na kuweza kununua vitendea kazi kwa ajili ya kuendelea kuboresha utendaji kazi wenu”,amesema Mhandisi Majala.
Ameongeza kuwa pikipiki hizo zitawawezesha CBWSO kufikia wananchi kwa urahisi zaidi, na kuwafanya waweze kutoa huduma za maji kwa wakati muafaka.
“Tafadhali, zitunzeni pikipiki hizi na mzitumie kwa mujibu wa sheria kwa malengo yaliyokusudiwa,” amesisitiza.
“Sisi kama serikali tunaendelea kuwapongeza kwa sababu nyinyi ni watekelezaji wakubwa wanaohusika na jamii ni CBWSO ambao nyinyi ndiyo mnaisaidia serikali kuhakikisha wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama”,amesema Mhandisi Majala.
Muonekano wa pikipiki kwa ajili ya Vyombo vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga.
Amesema pikipiki hizo zitawasaidia kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi , kwa wakati kwenye maeneo ya vijijini ili huduma ya maji ipatikane muda wote huku akiwataka wazitunze na wazitumie pikipiki hizo kwa mujibu wa sheria kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Niwapongeze kwa makusanyo makubwa ya maji tangu tujiunge na mfumo wa GePG. Naomba tuendelee kuwa walimu, mabalozi wazuri kwa watu wengine kwenye maeneo mengine kuhusu mfumo huu ambao umeleta manufaa makubwa. CBWSO Shinyanga mmekuwa mfano wa kuigwa, hongereni sana. Endeleeni kuwa wabunifu”,ameongeza Mhandisi Majala.
Katika maelezo yake, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, amefafanua kuwa kupitia mapato yao ya ndani, CBWSO imeweza kununua pikipiki zenye thamani ya shilingi milioni 23.9, na kuongeza idadi ya pikipiki kufikia 18.
“Katika kupunguza upotevu wa maji, tumenunua mita 840 zenye thamani ya shilingi 166,934,400.86/= za Bylan ambazo zina ufanisi mzuri zaidi katika kusimamia matumizi ya maji ukilinganisha na mita nyingi zinazotumika katika maeneo yetu, Tayari mita 443 zimepokelewa” ,amesema Payovela.
Muonekano wa pikipiki kwa ajili ya CBWSO Mkoa wa Shinyanga.
“Ili kuhakikisha kuwa skimu za maji zilizopo na zilizokamilika zinaendelea kutoa huduma ya maji endelevu, RUWASA Mkoa wa Shinyanga imeunda CBWSO 28 baada ya kufuta usajili wa CBWSO 43 zilizokuwa hazina uwezo wa kujiendesha. CBWSO hizi 28 zinahudumia skimu 181 za mtandao wa bomba na pump za mkono katika vijiji 383 kati ya vijiji 435 vinavyohudumiwa na RUWASA”,ameongeza.
Amefafanua kuwa, mwishoni mwa mwaka 2023 CBWSO zote 28 za mkoa wa Shinyanga ziliunganishwa kwenye mfumo wa Malipo kwa njia ya Kielektroniki (GePG) kupitia mfumo wa MAJI IS ili kuongeza ufanisi wa makusanyo ya maduhuli ya serikali yatokanayo na mauzo ya maji, na kuendelea kuboresha utoaji wa kuboresha huduma ya maji safi na salama.
“Manufaa yaliyobainika baada ya CBWSOs kujiunga na mfumo wa GePG ni pamoja na kuongezeka uwazi na udhibiti katika ukusanyaji wa fedha za umma kupitia dashboard ya vyombo CBWSOs. Kuongezeka kwa idadi ya wateja kutoka 8,144 hadi kufikia jumla ya wateja 10,041 ambao wote wamesajiliwa kwenye mfumo wa uchakataji wa Ankara za Maji (MAJI IS). Ankara zao zinachakatwa kwa njia ya mfumo na kupatiwa namba ya malipo (Control Number”,ameeleza Mhandisi Payovela.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela
“Tangu mfumo uanze kufanya kazi CBWSOs zote 28 hadi kufikia Juni 30, 2024 (Desemba 2023-Juni 2024) zimefanikiwa kukusanya shilingi 1,008,683,072.52/= ukilinganisha na sh. 676,821,904 kilichokusanywa kipindi cha Julai 2023- Novemba 2023. Ongezeko hili ni sawa na 49% (Tsh. 331,861,168.52/=”.
Jumla ya makusanyo ya mwaka 2023/2024 ni shilingi 1,685,504,976.52. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 CBWSOs zote zimekusanya jumla ya shilingi 662,073,893.46 kati ya shilingi 2,087,508,782/= kilichopangwa kukusanywa”,ameeleza Mhandisi Payovela.
Mwenyekiti wa CBWSO ya Mahembe wilaya ya Shinyanga Bw. Ndege Salu Nzala, amepokea pikipiki hizo kwa furaha, akisema zitawasaidia kufika kwa wakati katika maeneo yao ya kazi.
“Tunawashukuru RUWASA kwa kuendelea kutuunga mkono katika kazi zetu za kutoa huduma za maji vijijini,” amesema Nzala.
Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba huduma za maji safi na usafi wa mazingira zinapatikana kwa urahisi katika maeneo ya vijijini, na inathibitisha dhamira ya serikali ya kuboresha maisha ya wananchi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za msingi.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Makao Makuu, Mhandisi Mariam Majala akizungumza leo Jumatano Oktoba 16,2024 wakati akikabidhi jumla ya Pikipiki nane ambazo zimetolewa kwa Vyombo saba vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga ili kuboresha utendaji kazi wao. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Ufundi wa RUWASA Makao Makuu, Mhandisi Mariam Majala akizungumza leo Jumatano Oktoba 16,2024 wakati akikabidhi jumla ya Pikipiki nane ambazo zimetolewa kwa Vyombo saba vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela wakati wa makabidhiano ya Pikipiki nane zilizotolewa kwa Vyombo saba vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga ili kuboresha utendaji kazi wao.

Mkurugenzi wa Ufundi Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Makao Makuu, Mhandisi Mariam Majala akiwa amepanda kwenye moja ya Pikipiki nane zilizotolewa kwa Vyombo saba vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Ufundi Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Makao Makuu, Mhandisi Mariam Majala (kulia) akiwa akizungumza wakati akikabidhi pikipiki kwa Vyombo saba vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Ufundi Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Makao Makuu, Mhandisi Mariam Majala (kulia) akikabidhi funguo za pikipiki kwa Vyombo vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa CBWSO ya Mahembe wilaya ya Shinyanga, bw. Ndege Salu Nzala akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Muonekano wa pikipiki kwa ajili ya Vyombo vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa pikipiki kwa ajili ya Vyombo vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa pikipiki kwa ajili ya Vyombo vya Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CBWSO) Mkoa wa Shinyanga.
Hafla ya makabidhiano ya pikipiki kwa CBWSO Mkoa wa Shinyanga ikiendelea
Hafla ya makabidhiano ya pikipiki kwa CBWSO Mkoa wa Shinyanga ikiendelea
Hafla ya makabidhiano ya pikipiki kwa CBWSO Mkoa wa Shinyanga ikiendelea
Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge akizungumza wakati wa hafla hiyo
Picha za kumbukumbu wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki kwa CBWSO Mkoa wa Shinyanga