KAIMU Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma Dkt. Faudhia Mohamed,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma
Na.Gideon Gregory-DODOMA
KAIMU Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma Dkt.Faudhia Mohamed ametoa rai kwa wanawake kwenda katika Halmashauri kuchukua mikopo ya wakina Mama inayotolewa na Serikali ili kuweza kujikwamua kiuchumi pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika maeneo yao.
Dkt. Faudhia ameyasema hayo leo Oktoba 15,2024 jijini Dodoma wakati akiongoza Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika katika Kata ya Mpunguzi yaliyoongozwa na kauli mbiu inayosema “Wezesha mwanamke aishiye Kijijini kutumia nishati safi na salama, shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
“Twendeni Halmashauri tuchukue mikopo, hii mikopo ipo kweli na wenzetu wanafaidika nayo kwahiyo na nyie wanawake wa vijijini mkienda kukopa mtafaidika nayo mkienda kukopa nendeni kwa vikundi vyenu mkishachukua mtaongezea kwenye mitaji yenu kwasababu mwenye nacho anaongezewa,” amesema Dkt. Faudhia.
Aidha amewaomba wanawake hao kuhakikisha wanasimamia vyema suala la elimu kwa watoto wa kike ili waweze kujitete juu ya changamoto zinazowakabili katika jamii pamoja na kupatiwa haki zao za msingi.
“Baadhi yenu watoto wa kike hamuwapeleki shule mnawaacha wanakaa nyumbani wanafanya kazi za ndani hawapati elimu na hii ni shida kubwa sana wakikosa elimu wanashindwa kujisimamia kwahiyo sisi kama wazazi tunapaswa kuhakikisha watoto wetu wa kike wanapata elimu, “amesema Dkt. Faudhia.
Amesema kama wazazi wataona watoto wakike hawataki kwenda shuleni ni vyema wakaomba msaada kwa walimu kwani wapo kwa ajili ya kuwasaidia hivyo wasisite kuwafata ili suala hilo liweze kupatiwa ufumbuzi wa kina zaidi.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Milki ya Ardhi na Haki za Ardhi (LANDESA) Bi.Hadija Mrisho amesema kufuatia elimu wanayoitoa wamefanikiwa kuwezesha wanawake wengi waliopo Vijijini kumiliki ardhi kwa kiasi kikubwa kutokana na utambuzi walionao kwasasa.
“Suala la kumiliki ardhi linaanza na utambuzi kwasababu ukishatambua kwamba nina haki ya kumiliki na kupata ardhi pamoja na kufanya maamuzi basi utaweza kuhamka ili uweze kupata haki yako ya msingi ya kuanza miliki ardhi,”amesema.
Naye Wakili kutoka chama cha wanasheria wanawake Tanzania Bi.Isabella Nchimbi amewaomba watanzania kuheshimu haki za binadamu ikiwa ni pamoja na haki ya kumili ardhi ambayo kisheria kila mtu anayo haki hiyo licha ya kuwepo kwa mila kandamizi ambazo zimekuwa zikimnyima mwanamke kumiliki ardhi.
“Wote tunapaswa kuchukuliana sawa kwani binadamu wote ni sawa na kila mmoja anayo haki ya kumiliki ardhi hakuna sheria inayomzuia mwanamke au mwanaume kumiliki ardhi hata kwa kuangalia ni hali gani yuko nayo ya kimaumbile pamoja na vitu vingine,”amesema.
KAIMU Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma Dkt. Faudhia Mohamed,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma
KAIMU Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma Dkt. Faudhia Mohamed,akisisitiza jambo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
MWAKILISHI kutoka Shirika la Kimataifa la Milki Ardhi na Haki za Ardhi (LANDESA) Bi.Hadija Mrisho akizungumza na wanawake wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
WAKILI kutoka chama cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) Bi.Isabella Nchimbi akizungumza na wanawake kwenye Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
MWAKILISHI kutoka Shirika la WE EFFECT Bw.Frank Ademba,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
Bi.Zuhura Chimya akiongoza Mjadala wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
Innocent Nyambuya Diwani wa Kata ya Mpunguzi Mhe. Innocent Nyambuya ,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mdahalo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.

KAIMU Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma Dkt. Faudhia Mohamed,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuongoza Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
WASHIRIKI wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika leo Oktoba 15,2024 katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.