Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha ,Mussa Masaile akijiandikisha  kwenye daftari la mpiga kura katika kituo cha shule ya sekondari Sekei mkoani Arusha.
Happy Lazaro,Arusha .

Arusha .Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha ,Musa Massaile amewataka wananchi kufika kwenye vituo kwa ajili ya kujiandikisha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura katika shule ya sekondari Sekei day amesema kuwa yeye tayari ametimiza wajibu wake wa kujiandikisha katika kituo hicho.
Amesema kuwa,zoezi la kujiandikisha linaenda vizuri  kwani  mtu anafika tu  kituoni na kujiandikisha haichukui   hata muda mrefu .
“Nawaombeni sana wananchi wa mkoa wa Arusha mjitokeze  kwa wingi kwa ajili ya kwenda kujiandikisha kwenye daftari  hilo  na kuweza kupata haki zao za msingi .”amesema  Musa.
 Naye Mwandikishaji wa daftari la mpiga kura kituo cha shule ya sekondari sekei,Leah  Mgonja amesema kuwa  wamewahi  kituoni hapo kwa ajili ya zoezi hilo la uandikishaji  ambapo zoezi linaenda vizuri na mpaka sasa hivi hakuna changamoto yoyote.
Aidha amewataka wananchi mkoa wa Arusha kutumia nafasi hiyo kuja kujiandikisha kwani zoezi  hilo ni rahisi sana na hakuna kiambatanisho chochote wanachotakiwa kuja  nacho.