Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha ,Mussa Masaile akijiandikisha kwenye daftari la mpiga kura katika kituo cha shule ya sekondari Sekei mkoani Arusha.
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha ,Musa Massaile amewataka wananchi kufika kwenye vituo kwa ajili ya kujiandikisha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura katika shule ya sekondari Sekei day amesema kuwa yeye tayari ametimiza wajibu wake wa kujiandikisha katika kituo hicho.
Amesema kuwa,zoezi la kujiandikisha linaenda vizuri kwani mtu anafika tu kituoni na kujiandikisha haichukui hata muda mrefu .
“Nawaombeni sana wananchi wa mkoa wa Arusha mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya kwenda kujiandikisha kwenye daftari hilo na kuweza kupata haki zao za msingi .”amesema Musa.
Naye Mwandikishaji wa daftari la mpiga kura kituo cha shule ya sekondari sekei,Leah Mgonja amesema kuwa wamewahi kituoni hapo kwa ajili ya zoezi hilo la uandikishaji ambapo zoezi linaenda vizuri na mpaka sasa hivi hakuna changamoto yoyote.
Aidha amewataka wananchi mkoa wa Arusha kutumia nafasi hiyo kuja kujiandikisha kwani zoezi hilo ni rahisi sana na hakuna kiambatanisho chochote wanachotakiwa kuja nacho.