Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Ally Possi,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa Mwaka 2024/25 leo Oktoba 10,2024 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Ally Possi,(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa Mwaka 2024/25 leo Oktoba 10,2024 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Ally Possi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua wakati Mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa Mwaka 2024/25 leo Oktoba 10,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
OFISI ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndani ya Mwaka 2023/24, imeokoa zaidi ya Sh.Bilioni 602 na Dola za Marekani milioni 817.6 na Euro milioni mbili ambazo zingelipwa kwa wadaiwa endapo Serikali ingeshindwa kwenye mashauri hayo.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 10,2024 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Ally Possi,wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa Mwaka 2024/25.
Dk. Possi,amesema kuwa kwa kipindi hicho Ofisi imesajili na kuendesha ya mashauri ya madai 9,650 kati yake 9,519 ni ya kitaifa (zaidi ya asilimia 60 ya mshauri yakiwa ni migogoro ya ardhi) na mashauri 131 ni ya kimataifa.
“Katika kuendesha mashauri hayo, mashauri 1,412 yalimalizika ambapo Ofisi imeokoa Sh.Bilioni 536.51 na pia Ofisi imeshughulikia mashauri ya usuluhishi 201 ambapo, kati yake 170 ni ya usuluhishi wa ndani na mashauri 31 ni ya usuluhishi wa kimataifa.”
“Kati ya mashauri 201 yaliyoshughulikiwa, mashauri 43 yamemalizika kwa njia ya majadiliano, mahakamani na kwenye Mabaraza ya usuluhishi. Kumalizika kwa mashauri haya, Ofisi imeokoa Sh. Bilioni 66.02, Dola za Marekani 817,643,693.12 na Euro milioni mbili,”amesema Dk.Possi
Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Alice Mtulo ,amewataka wafanyakazi wa ofisi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi.
“Kati ya Julai 2023 hadi Juni 2024, watumishi 80 wamepata mafunzo ndani na nje ya nchi, pamoja na kuboresha ofisi kwa kuweka vifaa 69 vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ofisi za mikoa na makao makuu.”amesema