Mkuu wa shule ya wavulana Tengeru boys,Gaudence Mtui akizungumza kwenye mahafali hayo
Wahitimu wa kidato cha nne wakiimba nyimbo za kutumbuiza kwenye mahafali yao.

Happy Lazaro,Arusha .

Arusha .Wazazi wa  wanafunzi  wa kidato cha nne   na kidato cha pili wanaosoma katika shule ya sekondari ya  wavulana  Tengeru Boys iliyopo mkoani Arusha wamechanga kiasi cha shs 64 milioni kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa mitihani ambapo kiasi cha shs 1.344 bilioni kinahitajika kwa ajili ya kukamilisha jengo hilo.

Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkuu wa shule ya  wavulana Tengeru boys,  Gaudence  Mtui wakati akizungumza katika mahafali ya 17  ya wavulana Tengeru boys ambapo jumla ya wanafunzi 136 walihitimu yakiwemo  mahafali ya 4 ya Holy Ghost viziwi.

Mtui amesema kuwa mbali na wazazi hao kuchangia fedha hizo , Mamlaka ya hifadhi ya  Ngorongoro imewachangia kiasi cha shs 15 milioni  kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo ambapo linatarajia kuanza hivi karibuni na litaweza kuhudumia wanafunzi   mia mbili kwa wakati mmoja na kuondoa changamoto wakati wa kufanya mitihani.

“Jengo tulilokuwa tukitumia ni dogo  kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi iliyopo sasa hivi hivyo kukamilika kwa ujenzi huo utasaidia sana wanafunzi hao kuweza kutumia jengo hilo kwa ajili ya mitihani ambapo ukumbi huo utakuwa na ofisi nne na madarasa sita.”amesema .

Aidha amewataka wadau mbalimbali kusaidia juhudi hizo zilizoanzishwa na wazazi kwani wameonyesha mfano wa kuigwa kwa ajili ya  kusaidia watoto  wao kuwa na ukumbi huo .

Mtui amesema kuwa ,kumekuwepo kwa kiwango.kikubwa cha ufaulu shuleni hapo ambapo mitihani ya  Mock na CSSC  ambayo walifanya kikanda vijana wote walishika nafasi ya kwanza katika kanda ya kaskazini Magharibi inayojumisha mikoa ya Kulima,Arusha na Manyara. 

Ameongeza kuwa,kwa upande wa shule ya Holy ghost viziwi walimu  wanajitahidi  sana wakiamini  kuwa ulemavu sio kizuizi cha kufikia ndoto  ya mafanikio kwa vijana wetu wasiosikia, ambapo wahitimu wamekuwa wakipata daraja la kwanza mpaka daraja la tatu na vijana wote waliomaliza kidato cha nne  kati.ya 2021,2022,na 2023 walifanikiwa kuendelea na masomo katika ngazi zingine za kitaaluma kama kidato cha tano na vyuo vya kati.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika.mahafali hayo  Kamishna msaidizi mwandamizi mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Dk.Mariamu  Kobelo  amesema kuwa , shule hiyo  imekuwa ikiwalea watoto na kuwafundisha malezi mazuri ya kiroho sambamba na kuwafundisha kuhusu swala zima la maadili na kuweza kuepukana na vitendo viovu  hususani wanapokuwa mtaani. 

Amesema kuwa, kila  mmoja anashuhudia namna ya ambavyo kumekuwepo na mmomonyoko  wa maadili unaosababishwa utandawazi  ,hivyo nawaomba wazazi wajitahidi kuwa karibu na watoto wao kwani ndio  kwanza safari ya maisha imeanza .

“Nawaomba  sana wazazi mhakikishe mnawajengea watoto mazingira mazuri ya elimu.kwani elimu.ndio urithi pekee unaoweza kumpatia mtoto kwa ajili ya maisha yake ya baadaye”amesema Mariamu.

Nao baadhi ya wanafunzi waliohitimu masomo yao,Anthony Mushi na Abiri Rembo  wamesema kuwa shule hiyo imewaandaa  kuweza kujiajiri kutokana na kufundishwa masomo mbalimbali.kwa vitendo zaidi na kuweza kujifunza maswala mbalimbali ambayo yatawasaidia kwa maisha yao ya baadaye ikiwemo kuweza kuanzisha biashara mbalimbali.