Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake mkoani Ruvuma, uliofanyika leo Septemba 28,2024 katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Kilimo, kuanzia msimu ujao wa mavuno, kuhakikisha wakulima wanalipwa moja kwa moja na vyama vikuu vya ushirika badala ya utaratibu wa sasa wa kupitishia malipo hayo kupitia Vyama vya Msingi (AMCOS), ili kuondoa malalamiko ya wakulima kucheleweshewa malipo yao na kuongezewa makato.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake mkoani Ruvuma, uliofanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Rais Dkt. Samia pia amewasihi wakulima kutumia vizuri fedha za mauzo ya mazao wanayouza ili waweze kujikwamua kiuchumi na kupambana na umasikini.
Aidha amesema Serikali itaendelea na utaratibu wa Stakabadhi Ghalani, Soko la Bidhaa (TMX) na minanda kwa njia ya mtandao ili kumnufaisha mkulima moja kwa moja na kupata takwimu sahihi za wakulima kitaifa ili Tanzania isomeke katika ramani ya biashara ya kilimo na kuweka urari mzuri kwenye biashara ya kimataifa.
Kuhusu Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Rais Dkt. Samia amesema kuwa NFRA itaendelea kuimarishwa ili iendelee kuwa soko la uhakika la mazao ya nafaka na kulihakikishia taifa usalama wa chakula. Amesema kuwa Serikali imeweka mifumo itakayowezesha NFRA kununua tani 170,000 za mahindi kutoka kwa wakulima mkoani Ruvuma.
Kwa upande wa kilimo cha umwagiliaji, Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 50 ya kilimo cha Tanzania kitakuwa cha umwagiliaji maji. Ameeleza kuwa Mkoa wa Ruvuma pekee una miradi 33 ya umwagiliaji inayojumuisha ujenzi, ukarabari, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika skimu, mabwawa na mabonde katika Halmashauri mbalimbali za mkoa huo.
Hali kadhalika, Rais Dkt. Samia amesema Serikali inajipanga kuanzisha vituo vya zana za kilimo kwa kuanzia na mikoa inayozalisha chakula kwa wingi ikiwemo mkoa wa Ruvuma kwa kutoa vifaa na huduma za kilimo kwa ruzuku ili kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake mkoani Ruvuma, uliofanyika leo Septemba 28,2024 katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichanu),akizungumza wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake mkoani Ruvuma, uliofanyika leo Septemba 28,2024 katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Sehemu ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichanu),akizungumza wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake mkoani Ruvuma, uliofanyika leo Septemba 28,2024 katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.