MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Kidatu cha Sita wa Skuli ya Sekondari ya Ben Bella.Aisha Hamad Bakari,wakati akitembelea maonesho ya Wanafunzi, wakati wa hafla ya Mahafali ya Tatu ya Wanafunzi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Zanzibar,yaliyofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Unguja leo 28-9-2024 katika ukumbi huo.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia (KIST) Ndg.Hassan Hamad Yussuf,wakati akitembelea maonesho ya Wanafunzi, wakati wa hafla ya Mahafali ya Tatu ya Wanafunzi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Zanzibar,yaliyofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Unguja leo 28-9-2024 katika ukumbi huo.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Vyuo na Vyuo Vikuu Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA wakifuatilia hutuba ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika mahafali ya Wanafunzi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi huo leo 28-9-2024.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wageni waalikwa na Wanafunzi wakishangilia wakati Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Mahafali ya Tatu ya Wanafunzi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Zanzibar, yaliyofanyika leo 28-9-2024, katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika Mahafali ya Tatu ya Wanafunzi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Unguja leo 28-9-2024.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akionesha zawadi maalumu aliyokabidhiwa na Uongozi wa UVCCM, wakati wa Mahafali ya Tatu ya Wanafunzi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Zanzibar, yaliyofanyika leo 28-9-2024 katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Unguja, na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg.Mohammed Ali Mohammed (Kawaida) na (kushoto kwa Rais) Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg.Rehema Sombi Omary.(Picha na Ikulu)
….
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imeongeza bajeti ya Sekta ya Elimu ili kuwawezesha vijana zaidi kunufaika na mikopo na kuendelea na elimu ya juu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo, leo tarehe 28 Septemba, 2024 Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja kwenye Mahafali ya Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo vikuu Zanzibar, yaliyoandaliwa na (UVCCM), ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA).
Amesema, Serikali imeongeza bajeti ya Elimu kutoka TZS bilioni 265.5 kwa mwaka 2021/2022 na kufikia TZS bilioni 851 mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 221.
Rais Dk. Mwinyi amewahakikishia vijana wote wanaopata fursa ya kujiunga na elimu ya juu kuwa watapata mikopo isiyo na masharti na kueleza kwamba Serikali imeongeza bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzibar kutoka TZS bilioni 4.0 mwaka 2011 hadi TZS bilioni 33.50 mwaka 2024.
Amebainisha kwamba, kiwango hicho cha fedha kinawasomeshea vijana 7,367 wa elimu ya juu kwa kuwanufaisha wanaosoma vyuo vya ndani ya Tanzania na nje ya nchi.
Dk. Mwinyi amesema ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wananufaika na fedha hizo, tayari Serikali imeanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma ngazi za stashahada (Diploma).
Aidha, Dk. Mwinyi amewaelezea wanafunzi 365 wenye ufaulu bora zaidi wa daraja la kwanza wananufaika na ufadhili unaotolewa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini.
Kadhalika amesema, Serikali imeimarisha mafunzo ya amali kwa kujenga miundombinu imara ya fani za ufundi wa aina tofauti inayofundishwa kwa vyuo vya mafunzo ya amali nchini ili kuwajenga kiuweledi wahitimu wa vyuo hivyo wanapomaliza masomo yao wajiajiri na kuajiriwa.
Dk. Mwinyi pia amewataka vijana kutumia fursa ya elimu iliyopo kwa kujiendeleza pamoja na kuongeza maarifa ya kitaalmu waliyoyapata kipindi cha mafunzo yao.
Akizungumzia ujenzi wa vyo vikuu, Rais Dk. Mwinyi amesema tayari Serikali imeanza ujenzi wa vyuo vyengine vipya vitano vya mafunzo ya amali Unguja na Pemba ili kutoa fursa zaidi kwa vijana wengi kupata ujuzi na maarifa ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira.
Alisema, ujenzi wa vyuo hivyo ni jitihada za Serikali anayoiongoza za kuimarisha uwekezaji kwenye huduma za jamii na ujenzi wa miundombinu ikiwemo ya barabara, viwanja vya ndege, bandari, masoko na kuhamasisha wawekezaji wa sekta ya utalii na ujenzi wa viwanda, ni miongoni mwa dhamira za kuongeza fursa za ajira na kukuza uchumi wa nchi.
Akielezea mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake hususan kwenye sekta ya ajira, Dk. Mwinyi amebainisha jumla ya miradi 330 yenye mtaji wa dola za Marekani bilioni 5.4 imesajiliwa na kutegemewa kuzalisha ajira zaidi ya 18,000 kwenye sekta ya uwekezaji na shughuli za biashara.
Alisema, juhudi hizo zinakwenda sambamba na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi wakiwemo vijana kupitia “Programu ya Inuka” ambapo Serikali iliweka TZS bilioni 15 za mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa kwa wananchi.
Pia alisema, tayari mikopo yenye thamani ya TZS bilioni 30.2 imetolewa kwa wananchi kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 sambamba na kueleza kuwa Serikali imetenga jumla ya TZS bilioni 41.6 kwa lengo la kuongeza fedha za kutoa mikopo katika awamu ya pili ya “Programu ya Inuka”.
Pia, Dk. Mwinyi ametoa wito kwa vijana kuendelea kuzitumia fursa mbalimbali zinazoandaliwa na Serikali kupata elimu pamoja na fursa za kujiendeleza kiuchumi.
Aidha, ameeleza mpango wa Serikali wa kuendelea kuimarisha fursa kwa vijana ikiwemo elimu na mafunzo, kuwapatia mikopo na kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo binafsi kwaajili ya vijana na Taifa kwa jumla.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.