Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Felician Mtehegerwa akizungumza katika mahafali hayo mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa shule hiyo ,Naomi Masenge akizungumza kuhusiana na mahafali hayo mkoani Arusha .
Happy Lazaro,Arusha .
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili kwa kuhakikisha wanatoa taarifa kwa vyombo husika ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Aidha amewataka kuwa mstari wa mbele kuwafichua wale wote wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwani vinasababisha madhara makubwa kwa watoto.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Felician Mtahengerwa wakati akizungumza na wazazi katika mahafali ya ya 14 ya shule ya mchepuo wa kiingireza ya Tuishime iliyopo mkoani Arusha .
Mtehengerwa amesema kuwa ,kumekuwepo na changamoto kubwa katika.jamii ya kuporomoka kwa maadili kwa kiwango kikubwa ambapo jamii yenyewe imekuwa ikifanya vitendo vya ukatili bila kuwa na hofu yoyote.
“Nawaombeni sana wazazi kila mmoja asimame kwa nafasi yake kukemea vikali vitendo hivyo kwani wanaofanya hivyo tupo nao kwenye jamii na tunawafahamu vizuri ,hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunakemea vitendo hivyo na kuwa mstari wa mbele kuyaripoti sehemu husika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua mara moja.”amesema Mtehengerwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo ,Naomi Masenge amesema kuwa ,shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kila mwaka na hiyo ni kutokana na walimu waliobobea vizuri katika.masomo mbalimbali .
Amesema kuwa ,wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa katika maadili mema ambapo pindi wakihitimu masomo yao wamekuwa ni mfano mzuri wa kuigwa katika.jamii kutokana na kufanya vizuri kitaaluma na kuwa na maadili mazuri wanayofundishwa shuleni hapo .
“Tumekuwa tukifundisha masomo ya ziada ambayo ni somo la kompyuta na kifaransa ,na tunaomba wazazi wazidi kufuatilia na kuendeleza ndoto za watoto wao ambazo wamezianzisha shuleni kwani walienda shule nyingine wanazidi kufanya vizuri zaidi “amesema Masenge.
Nao baadhi ya wadau wa elimu jiji la Arusha waliiomba serikali kukomesha magenge ya watu wanaojihusisha na matukio ya utekaji wa watoto na kuwafanyia vitendo vya ukatili ili waweze kukomeshwa na kuchukuliwa vitendo vya kisheria .
Aidha baadhi ya wahitimu wa darasa la saba ,wamesema kuwa,wamefurahi kwa namna ambavyo.shule hiyo imekuwa ikiwaandaa kuweza kujitegemea pindi wanapomaliza shule kwa kuwafundisha masomo ya ujasiriamali ambayo huwawezesha kujitegemea sambamba na kuwafundisha nidhamu .